Download Mwanachuo planner ili uandike malengo yako ya chuo sasa

Your Guide To University Life / Maisha ya Chuo

Makosa niliyoyafanya nilipokuwa chuo | Your Guide to University Life

Reading Time: < 1 minute

Nianze na lipi, maana….

Kwanza kama bado haujafollow Instagram page ya Maisha ya Chuo embu fanya hivyo Bonyeza Hapa.

Haya tuendelee na makosa niliyoyafanya :

1) Kutokusave hela ya boom na nilizokuwa natumiwa nikiwa chuo

I wish ningesave kiwango fulani cha boom au hela ambayo mzazi alikuwa akinitumia (ukiwa chuo utatumiwa hela kwasababu wanajua unazihitaji sana), au kuliingiza kwenye biashara inayoendelea hadi nikimaliza chuo. Kwasababu sasa hivi najisikia kama naanza upya na maisha wakati nilikuwa na hela nyingi kipindi kile.

Bonyeza Hapa Kupata Idea za Biashara ambazo unaweza kuzifanya chuo

2) Kupoteza muda kwenye mahusiano

Na kuumizana. Kiukweli mahusiano mengi ya chuo hayadumu, Ila hilo halina maana yote, wengine hudumu. Ila nilijikuta nimedate wengi haswa kwa vile niliaminishwa usipopata mtu chuoni hautopata tena maishani, kitu ambacho sio kweli. Kwahivyo nilijikuta nikiweka effort kutafuta hayo mahusiano hata nilipoona hakuna mwelekeo, nakupoteza muda ambao ningeutumia kuufanya mambo mengine.

3) Kutokujali na kuweka effort sana kwenye masomo

Mimi ni kati ya wale waliokuwa wanajua chuo ni bata, na of course nilienjoy na nimefaulu vizuri, ila sikuweka effort kama niliyokuwaga nayo nilipokuwa sekondari. Ni vile sikujua/sikujali kwamba matokeo yangu yanaumuhimu miaka yote, nilidhani matokeo yalikuwa yana umuhimu mwaka wa mwisho tu.

4) Kudoji darasani

Guys, nilikuwa doja sana. Na sio tabia nzuri kwasababu nilipata hadikesi kwasababu ya kudoji darasani. Kiukweli simshauri mtu oyote adoji darasani sio jambo zuri kabisa na linaweza kukucost.

Hayo ni makosa machache kati ya mengi niliyowahi kuyafanya nikiwa chuo, ambayo sitamani na wewe upitie huko.


Kama ungependa niwe msaada wa karibu kwenye maisha yako ya chuo, hakikisha una SUBSCRIBE kwenye channel yangu inayohusu maisha ya chuo tu, nitashare jinsi ya kubalance masomo na fun, jinsi ya kudeal na stress za chuo na kujibu maswali yote yanayohusu chuo..

Link hii hapa https://www.youtube.com/c/maishayachuo

Eunice

6 Comments

Share Your Thoughts With Me