Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Jinsi ya kufikia malengo/ndoto yako

Hii topic naandika kutokana na discussion niliyokuwa nayo leo na vijana wenzangu wa Mwanza, ambapo tulidiscuss mambo tunayodhani yataweza kutusaidia kufikia malengo yetu. Kwasababu ukweli ni kwamba, Mimi pia sijafikia malengo yangu kwahiyo ingekuwa suala la kushtua sana kuleta njia kama vile nimefika.

Kwahiyo moja kwa moja nielezee point tulizoziongelea:

Kuanza pale ulipo

Kuna mmoja alitushirikisha vile anandoto ya kuja kufungua kituo cha watoto wasiojiweza na kuwasaidia. Ila kwasasa kila akitoka home huwa anawapa watoto anaokutana nao mtaani hela yoyote ndogo aliyonayo mkononi. Kwahiyo ingawa kwasasa bado hajafungua kituo, bado anasaidia watoto kwa uwezo alionao pale alipo… Vunja ndoto yako iwe kwenye vindoto vidogovidogo ambazo unaweza kuvifikia step by step.

Kuwa na role model na mentor

Kuna mmoja anatamani kuwa mwanajeshi kama mjomba wake. Na kuna tofauti ya role model na mentor, ambapo role model unamuona sehemu alipo na kutamani kufikia, Ila mentor anakuwa sehemu uliyopo au yuko vizuri eneo unalotamani kujua zaidi, halafu yeye anakusaidia na wewe ujue kile anachojua. So ukitaka kufikia malengo yako unahitaji wote, ingawa mwenzetu amepata vyote kutoka kwa mtu mmoja.

Kuwa kimbelembele na kutumia kila nafasi inayokusogeza karibu na ndoto yako

Kuna mmoja alisema anatamani kuwa DJ, kwahiyo kama event haina DJ, kwasasa haangalii sana malipo anaangalia ujuzi lakini pia hawezi jua akachukua hiyo kazi ambayo anaona haina malipo na akaonwa na nani ambaye atamsaidia vipi kwenye hiyo ndoto yake. Kuwa kimbelembele, kuacha woga na kujitoa ni jambo la muhimu katika kufikia malengo.

Kuwa na imani na kujiamini

Kuwa na imani inaendana na kuwa na mawazo chanya hata kama matatizo yatatokea. Kujiamini ni kujua kuwa unaweza, kujiongelea maneno chaya na kujiangalia kama mtu ambaye anaweza kufanikiwa katika hilo lengo ulilonalo.

Kuwa na mipango

Tuliongelea vile ukiwa na lengo halafu usipopanga hatua ya jinsi ya kulifikia hautolifikia, unaweza kuweka mipango wa hela kama ndoto yako inategemea hela (kwahiyo unaweza kuweka akiba kwaajili ya hiyo ndoto) au ukaweka mpango wa mazoezi, nk.

Related : Fursa za Biashara Unazoweza kuzifanya | Idea za Biashara

Consistency

Kuendelea kuifanya ndoto yako (kufanya kila linalotakiwa kufikia ndoto yako, to show up everyday for your dream).

Support

Tuliongelea kwanini wasanii wanakuwa na marafiki au vikundi na wasanii wenzao, hii yote ni kwasababu watu wenye ndoto sawa na wewe wanakuelewa zaidi ya wale ambapo hawana ndoto sawa na wewe. Lakini pia watu wenye ndoto sawa na wewe, watakupa vitu vipya ambavyo wanajifunza nawe utawapa vitu vipya, kwahiyo unazidi kukua.

Resilience

Ni ile tabia ya kukutana na matatizo lakini bado ukanyanyuka na kuendelea mbele, yani umepigwa mara saba, ya nane unainuka. Kutokugive up, kuinuka kila unapokutana na kikwazo.

Jua kuwa utakutana na vikwazo

Be realistic, utakutana na vikwazo mbalimbali katika njia yako ya kufikia ndoto yako, ukijua hili litakusaidia kujiandaa kisaikolojia. Kuliko kuamini njia itakuwa haina mabonde halafu ukakutana nayo ukaamua kurudi nyuma.

Self control / discipline / commitment

Kujicommit ili kufikia ndoto yako, lakini pia kujicontrol usifanye vitu ambavyo vitakufanya usifike (mfano: kuvuta madawa nk), lakini pia kuwa na discipline ili kufikia malengo… Kuheshimu ndoto yako na kufanya kila effort ili kufikia.

Kujua mwisho wa ndoto yako

Ukweli ni kwamba kwenye maisha ukifikia ndoto moja, utatengeneza nyingine. Tuliongelea kuifanya ndoto yako kubwa iwahusishe watu wengine, yani ukifanikiwa, wawe wamefanikiwa wengi kwa kufanikiwa kwako. Hii inasaidia kwasababu hauoni hii ndoto ni yako tu kwahiyo unaweza ukaiacha, Ila unaona wale watu watakaofaidika nayo pia.

Na hayo ndo mambo ambayo tuliyaongelea, ni katamani nikushirikishe na wewe.

Eunice + Mwanza youth

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป