Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

anonymous person with binoculars looking through stacked books
Guest Post

Mambo 3 ya muhimu katika maisha ambayo inabidi uwe makini unapoyatafuta

Katika maisha ya mwanadamu, yapo mambo mengi ambayo huvuta umakini wa kila mtu. Miongoni mwa mambo hayo yapo mambo matatu ambayo kutokana na takwimu za utafiti nilioufanya yameshika na kukamata hatamu ya umakini wa maisha ya mwanadamu. Mambo haya matatu yamepelekea kuwepo na matapeli wengi sana katika nchi mbalimbali tena mambo haya yameongeza udanganyifu mkubwa katika maisha.

Mambo haya matatu kila ukipita katika maeneo mbalimbali mjini utakutana na vibao vinavyotaja kuhudumia watu katika mambo hayo. Tena wametokea wachungaji na wahubiri wengi wakiyapa kipaumbele mambo haya kwa sababu ndio yanagusa maisha ya mwanadamu kwa asilimia zaidi ya 90%. Zaidi wakaibuka mitume na manabii wa kila aina wakifungua makanisa yao na kuwahubiria watu juu ya mambo haya matatu.

Katika haya mambo matatu watu wengi wamejiingiza katika dhambi  na kumkana Mungu katika kuyatafuta. Leo nataka tuyazungumzie kwa undani sana ili tujue namna ya kuyatafuta kwa njia halali huku tukimtumikia Mungu.

faceless woman inserting credit card into subway ticket machine

Mambo hayo ni, Mafanikio, Umaarufu na Upendo.

1- Mafanikio

Maneno ya Mungu yanasema tujitabirie makubwa na ushindi na wengi huwa tunawaza mafanikio tu. Mungu alituumba ili tuwe washindi. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu duniani wanapenda kufanikiwa na wana malengo ya kufika mbali ingawaje watu wanaoambatana nao ndio wanaowakwamisha wasifike mahali walipoumbiwa kuwa kwa wakati.

Wamejitokeza waganga wa kienyeji wakizungumzia suala la mafanikio  na wakiahidi kumpa mtu mafanikio pindi atakapofuata matakwa yao. Ni kweli unaweza ukafanikiwa kupitia watu hawa lakini mafanikio yao ni ya majuto na ni ya muda tu, mafanikio ya kweli yanatoka kwa Mungu.

Leo nataka nikuambie wengi huwa wanalaghaiwa kwa kutumia sehemu hii ya mafanikio katika maisha. Watajitokeza watu wa namna mbalimbali ili kukuvuta katika njia mbalimbali za mafanikio lakini kabla haujaingia katika njia hizo hebu jipime katika sifa nne za watu wenye kufanikiwa katika maisha; a) Watu wanaofanikiwa siku zote huwa na hamu ya kufanikiwa zaidi ya wengine hivyo kuweka juhudi kubwa katika kazi.

b) Ni watu wanaopenda matokeo ya mafanikio yao yawe yametokana na jitihada zao na Mungu wao

c) Ni watu wanaosonga mbele aidha wamefanikiwa au hawajafanikiwa, aidha wamekubaliwa au wamekataliwa, wana imani kubwa katika neno “siku moja nitashinda”

d) Ni watu wanaopenda kuanza na kazi ngumu kwanza kisha kumaliza na zile nyepesi, huwa na vipaumbele makini sana katika maisha yao.
Kuna namna zitakuja kwa uzuri na ubora kabisa lakini ndani yake zimejaa dhambi cha kufanya ni kuwa makini.

Pia Soma : Sheria 7 za mafanikio

2- Umaarufu

Jambo lingine ambalo limekamata watu wengi ni unaarufu. Watu wa kila aina wamekuwa wakitafuta umaarufu kwa njia mbalimbali, wengine wameamua mpaka kumwabudu shetani ili tu wawe watu maarufu na tunawajua, wengine wameamua kuwa waasherati wa viwango vya lami ili tu wajulikane na watu, wengine wamejidhalilisha na kukaa hadi utupu mbele za watu ili wawe maarufu na wengine wamejitoa miili yao ikatumiwa na watu ambao waliwaahidi kuwashika mkono ili wawe maarufu.

Watu wanaotumia nguvu zote ili kuwa maarufu huku wakimwacha Mungu huishia mahala pasipofaa maana ujira wao wanakuwa wameshaupata,

man performing on stage

3- Upendo/ Mapenzi

Kila ukipita mitaani utakutana na mabango ya waganga yanayotangaza kutoa huduma za kukuza uchumi, kurudisha wapenzi, kufanya mtu awe maarufu. Wengine ni manabii na mitume nao wamejikita katika mambo hayo hayo na wanavutia watu wengi mnooo, vyombo vya habari na runinga vituo mbali mbali vya utangazaji asilimia kubwa ya vipindi vyao ni vyenye mada hizo tu. Hapa ndipo utagundua kwamba mwanadamu wa leo amekamatwa sana na haya mambo matatu.

Pia Soma : Mambo yanayotoke kanisani yanayonipa maswali magumu kuhusu ukristo

Wengi ambao wamekurupuka kutafuta mteremko katika mambo haya wameishia kujiingiza katika uasherati, uchawi, zinaa, vitendo vya wizi na kushindwa kupata thamani stahiki waliyoumbwa wawe nayo.

Wakati unapofikiria  kuvitafuta vitu hivyo vitatu kuwa makini sana maana kuna mazingira yatakuja kwa uzuri kabisa lakini usipokuwa makini yatakuangusha na kukufanya ushindwe kufika mahali ulipopaswa ufike. Umakini unahitajika sana, najua unahitaji kufika mbali sana, Mungu akusimamie ufike mahali unapostahili kufika.

Ubarikiwe sana!


Imeandikwa na Yuris Dutch, yurisdutch@gmail.com

Share Your Thoughts With Me

Translate »