Watu wengi hujiingiza kwenye biashara chuoni kwasababu mbalimbali. Wengine hawana boom, wengine wanatafuta kipato cha ziada, wengine wanamoyo tu wa ujasiriamali na sababu yoyote ile inayokufanya ufikirie kufanya biashara.

Kama biashara ni kitu unapenda kufanya ila hauna idea ya biashara ya kuifanya chuoni ambayo haikupotezei muda, hizi hapa idea za biashara chuoni;

Kabla haujaanzisha biashara chuoni, haya ni mambo ya muhimu kuyajua;

  • Hauwezi kufanya kila kitu peke yako, unahitaji msaada kutoka kwa watu, iwe roommate au mtu utakayemuajiri
  • Zingatia sababu ya kuanzisha biashara na malengo uliyonayo kuhusu hiyo biashara; je unataka tu hela ya kula au unataka hiyo biashara iwe kitu cha muda mrefu hata ukimaliza chuo ikuendeleze mtaani? Na kama ni hivyo una malengo gani ya kuikuza?
  • Jua jinsi ya kubalance muda vizuri kati ya masomo yako, biashara yako na maisha yako ya kijamii. Kujua zaidi kuhusu time management chuoni, BONYEZA HAPA.
  • Kufeli ni sehemu ya kujifunza, biashara inakufanikiwa na kujifunza. Usijisikie vibaya au aibu kufeli, usiogope kufeli, unajifunza vitu vya muhimu ambavyo usingeweza kujifunza kama unsingejaribu.
  • Zingatia kilichokupeleka chuo kama namba moja kwako, na hicho ni kusoma. Wewe ni mwanachuo mwenye biashara sio mfanyabiashara anayesoma chuo.

Usiogope kuanzisha biashara chuoni, usiogope hasara, unajifunza mengi kwa kufanya kuliko kuwaza tu au kuona wengine wakifanya. Ila zingatia tu kuwa ni muhimu pia kufocus kwenye masomo pia hata kama hela inaingia vizuri kwenye biashara.

Eunice

You May Also Like

1 Comment

  1. Jinsi ya kubalance kusoma na kufanya mambo mengine chuoni - Eunice Tossy

    […] Soma : Mambo 5 ya kuzingatia unapotaka kuanzisha biashara chuoni […]

Share Your Thoughts With Me

Translate ¬Ľ