Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Career Guide,  Guest Post

Makosa ambayo wahitimu wapya hufanya wanapopata kazi

Makosa ambayo wahitimu / waajiriwa wapya hufanya ofisini au kwenye maisha yao wanapopata ajira kwa mara ya kwanza;

1. Kuishi juu ya kipato chao (kuongeza standard ya maisha yao mara tu wanapopata kazi)

2. Kutokuweka akiba kwa kuona kuna mshahara unapatikana kila mwezi

3. Kukopa bila mradi na haraka/mapema tu baada ya kuajiriwa

4. Kubadilisha makazi haraka

5. Kuishi kwa kusubiria mpaka mwisho wa mwezi (unatumia hela mpaka hapo katikati unabakia kuangalia tarehe ya mwisho wa mwezi inafika lini)

6. Kuanza mahusiano mapya mapema tu baada ya kupata kazi na pia kuwa na mahusiano na watu wa ofisini (ofisi nyingine zinakataza mahusiano ya wafanyakazi)

7. Kuridhika

8. Kutokuridhika

9. Kutaka kuwa sawa na waliokutangulia

10. Kutaka kurahisisha kazi kuliko uhalisia

11. Kudharau watu wa chini yako

12. Kukosa utayari wa kujifunza zaidi kutoka kwa watu

13. Kuweka maslahi juu ya utu

14. Kuamini watu blindly

15. Kushindwa kutenganisha mambo ya kiofisi na mambo yako binafsi ama kujua jinsi ya kuwa na uwiano wa muda unapofanya mambo yako binafsi na ya kiofisi

16. Kushindwa kupumzika na hivyo kuathiri afya yako ya akili

17. Kuishi leo kesho, na kesho leo.

18. Kuogopa kuhisi haujui kitu, wakati unaweza kuuliza maswali au kujifunza

19. Kujihisi haustahili kuwepo ofisini na kuwa watagundua kuwa wewe unaigiza/unaungaunga tu/haujui unachofanya. Jiamini

20. Kuchukua mkopo kununua gari mara tu ukipata kazi, sio vizuri sana kujiingiza kwenye mkopo kwa haraka hivyo. Lakini pia kuwanunulia watu na kila mtu zawadi na vitu mbalimbali bila mpangilio kwa vile sasa una hela.


Kama una mambo mengine uliyoyaona tushirikishe kwenye comments


Moyo + Eunice

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป