Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Vitu 5 ambavyo natamani ningevijua nilipokuwa chuo

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Nimesoma miaka minne chuoni, nimehitimu mwaka 2018, degree ya Mechanical Engineering.

Kuna muda nikiangalia nyuma kuna vitu vingi ambavyo natamani ningevifanya tofauti au ningevifanya kwa moyo zaidi.. na ndio sababu nimeanzisha Maisha ya Chuo ili kushea vitu vilivyonisaidia, makosa niliyofanya na ujuzi wangu kuhusu Maisha ya Chuo ili wewe ufanikiwe zaidi yangu, uwe na msaada wa karibu usijihisi uko peke yako lakini pia uepuke pale nilipoteleza.

Leo naenda kukushirikisha mambo ambayo natamani ningeyajua nilipokuwa chuo, nayo ni;

Mahusiano mengi ya chuo hayadumu

Toka nimalize chuo ndoa ninazozijua za mahusiano ninayoyajua hazizidi mbili. Lakini watu tulifeli masomo, tulipata msongo wa mawazo, tulishindwa kusoma, kulala nk kwaajili ya vitu vilivyoisha. Najua hayo ni maisha ila ukilijua hili na kulikubali linaweza kukusaidia kujua wapi kwa kuwekeza nguvu.

Usijipe moyo kuwa wewe ndio unaweza ukadumu, kama ipo ipo tu kwasasa wekeza kwenye masomo kwanza.

Kudoji darasani kuna gharama sana

Labda siku nitawasimulia stori ya kesi niliyoipata kwasababu nilidoji lecture, wakawa wamebadilisha ratiba ya test nikakosa kuifanya. Usidoji darasani, kuna madini lecturer anatema darasani unaweza kuyakosa.

Kujiandaa na maisha ya mtaani mapema

Ni muhimu ukiwa chuo kufikiria chuo kwanza lakini pia kuwaza au kuwekeza kwaajili ya maisha yako ukija mtaani ni muhimu. Wengi hupata msongo wa mawazo maana wanaanza kuwaza kuhusu hili mwishoni wanapomaliza au mwaka wa mwisho. Ila ni muhimu kujiandaa kuhusu maisha yako ya mtaani toka ukiwa chuo, kufikiria taratibu jambo ambalo ungependa kufanya.

( Kama unafikiria kujiajiri baada ya chuo, haya hapa ni maamdalizi unayoweza kuyafanya ukiwa chuo – BONYEZA HAPA)

Kusave hela ya boom kidogo

Au hela yoyote unayoipata, utahitaji nauli kwenda kwenye usahili ukiwa mtaani, utahitaji pedi nk. Hela unayoipata chuo kutoka kwa wazazi au boom jitahidi uweke akiba kwaajili ya hata mwaka wako wa kwanza mtaani.

Naelewa kama hali ni ngumu pia, kwahiyo usijibane tu kisa nimesema. Ila nilitaka tu ujue jambo hili.

GPA na ujuzi vina maana mtaani

Nakumbuka tulipokuwa chuo kuna jamaa alikuwa anashinda workshop mara nyingi kujifunza, tulikuwa tunamcheka na kuona anapoteza muda au anajifanya kipanga. Ila ukweli ni kiwa yule ndio ametoka na ujuzi mwingi sana wa kozi kuliko sisi tulioridhika na theory na practical kidogo.

Chuoni jitahidi ujifunze zaidi mwenyewe. GPA ina umuhimu hata kwenye kuapply Masters, au Post Graduate ni mambo wanayoulizia pia.

Sio tu ya mwaka wa mwisho wanayoiangalia, wanaangalia overall, average. Kwahiyo tilia mkazo miaka yote.

Na hivyo ndivyo vitu ambavyo natamani ningevijua toka nipo chuo.


Follow @maishayachuo Instagram, ambapo nashea dondoo mbalimbali zinazokusaidia kwenye mambo mbalimbali kuhusu chuo.

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป