Bila kujua kutoa na kupokea ushauri ni sehemu ya maisha yetu. Yani inatokea kwa ukawaida sana kiasi kwamba muda mwingine huwa hatutilii maanani uzito wa jambo kama ushauri.

Ushauri unaweza kubadiisha maisha yako. Kwa wema, au kwa ubaya. Ushauri una nguvu sana. Hivyo ni vyema kuzingatia machache haya unapotoa au unapopokea ushauri :

 • Muda mwingine sio lazima utoe ushauri, muda mwingine sikiliza tu ili kumuelewa mtu
 • Ni vizuri kupokea ushauri kutoka kwa watu ila ni bora zaidi kama anayekupa ushauri amepitia hiyo hali unayoiongelea, ni rahisi sana ukiwa nje kujua linalotakiwa kufanya kwenye njia fulani kuliko ukiwa umevaa hivyo viatu unapita hiyo njia.
 • Unapotoa ushauri hakikisha moyoni unamawazo mema kwaajili ya huyo mtu/ unapopokea ushauri hakikisha unapokea kutoka kwa mtu anayekuwazia mema wewe (ni rahisi mtu kukupa ushauri huku akijifikiria kuwa hali yako inamuathiri vipi yeye kuliko kukufikiria wewe, hivyo jua kuchuja)
 • Pokea ushauri kutoka kwa yule unayejua unatamani kwenda alipo au ana lengo la kwenda mbali pia / usipokee ushauri kuhusu ndoto yako na njia za kupita kwa mtu ambaye anaelekea safari tofauti na hiyo.
 • Mtu akikuomba ushauri haimaanishi ni mjinga, usimfokee kiukali ukiwa na maana ya kumshauri, ongea naye kwa upendo, kwa kuona uzito wa lile alilokushirikisha.
 • Pokea shauri nyingi lakini mwisho wa siku akili ya kuambiwa ongezea na yako. Kaa chini fikiria mwenyewe.

Upo umuhimu wa ushauri, upo umuhimu wa wewe kushauriwa na kuwa mtu unayeshaurika yani unayepokea ushauri.

Kuna msemo unasema mtu mwenye akili hujifunza kupitia makosa yake, mtu mwenye hekima hujifunza kupitia
makosa ya wenzake.


Kuwa mtu unayeshaurika ni jambo jema sana maana linakusaidia kuepuka makosa mengi kwa kusikiliza ujuzi wa wengine lakini pia kupata hekima nyingi kwenye safari fulani kwa kupitia miongozo ya wengine. Lakini zingatia mambo hayo unapopokea / unapotoa ushauri.

Kwa kujua umuhimu wa ushauri, toleo la kwanza la gazeti la kidijitali la Stori za Bongo tumeshea stori mbalimbali za watu na ushauri ambao wamewahi kuupokea ambao umebadilisha maisha yao.

Stori za Bongo ni gazeti la kidijitali, yani unalisoma kwenye simu au vifaa vyako vya kidijitali kama laptop nk.

Ni gazeti ambalo linatoka mara mbili kwa mwezi likishare stori mbalimbali za wabongo wakijibu swali linaloendana na hoja ya toleo hilo, kwa toleo la kwanza walikuwa wanajibu kuhusu shauri walizozipokea na jinsi zilivyobadilisha maisha yao, toleo la pili tutaongelea hoja nyingine.

Kwenye gazeti hili wewe mTanzania ndio unashea stori yako, kwa maana stori yako inaweza kubadilisha maisha ya mwingine.

Sasa unaweza kupakua toleo la kwanza bureeee kabisa, au kulisoma mtandaoni bila kulidownload.

Bonyeza hapa kama unataka kulidownload👇🏿👇🏿

Bonyeza hapa kama unataka kulisoma chap chap mtandaoni bila kudownload👇🏿👇🏿

Hakikisha unafollow @storizabongo Instagram ili kupata hoja ya toleo la pili ili na wewe upate kushiriki toleo lijalo au kufuatilia @storizabongo kwa stori nyingi za wabongo zinazoweza kubadilisha maisha yako.

Eunice

You May Also Like

4 thoughts on “Mambo 6 ya kuzingatia unapotoa au unapopokea ushauri

 1. Jinsi ya kujali afya yako ya akili / vyakula, mitandao ya kijamii nk – Eunice Tossy

  […] Kwenye toleo la kwanza la Stori za Bongo nilishare stori mbalimbali za ushauri ambao watu wamewahi kupokea… kwenye toleo la pili nimeshare aina mbalibali za magonjwa ya akili, jinsi ya kujali afya yako ya akili na vyakula vizuri kwa ajili ya afya ya akili. […]

 2. Sababu 6 zinazowafanya watu wafeli kwenye maisha – Eunice Tossy

  […] Pia soma : Mambo ya kuzingatia unapotoa na kupokea ushauri […]

 3. Hii ndio sababu mitaji mingi ya biashara mpya hufa mapema – Eunice Tossy

  […] Pia Soma : Mambo ya kuzingatia unapotoa na kupokea ushauri […]

 4. Why I walked out on Christian women’s ministries – Eunice Tossy

  […] Women ministries are built on the idea that men love the same type of women and they have the same type of behaviors, and if you become a certain type of a woman, a man will love you, if he hasn’t well you are not yet that type of a woman sis, you are failing. They don’t care about personalities or learning more about you, they are about fixing you to be a certain type of a woman, they are not about god’s experience, they are about what the teacher wants to teach you about what she has been through, forgetting that life experiences are diverse. Don’t get me wrong it is good to learn from others, but what someone else goes through doesn’t n… […]

Share Your Thoughts With Me

Translate »