Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post

Jinsi ya Kuwa Mpenzi Bora

Katika mahusiano, kila mmoja wetu hupenda kuwa bora kwa mpenzi wake – inaweza isiwe bora kabisa lakini angalau kujitahidi kuonyesha kuwa unataka kuwa mtu aliye bora kwa mwenzi
wako.

Hii yote ni katika kutaka kudumisha mahusiano yenu.

Katika ulimwengu ambao mioyo ya wengi haina imani juu ya mahusiano yaliyo bora, Unaweza kuwa mpenzi bora kwa kufanya mambo yafuatayo…

Kuwa muwazi

Usitegemee mwenzio agundue unachofikiria bali funguka – mueleze kile unachojisikia, mwambie kile ambacho haukifurahii kutoka kwake na muombe ajaribu kurekebisha – epuka lugha za lawama na kukata tamaa.

Jenga amani ya kweli na si amani feki/uongo

Amani ya kweli itakusaidia kuona makosa na kuyatatua kwa faida ya wote.

Usiwe na amani ya uongo – kwa mfano unaona kabisa mwenzio anakukosea halafu unaamuna kukaa kimya kwa kuogopa ukimwambia atachukia.

Huko ni kutengeneza amani ya uongo wakati unaumia kwa ndani.

Jenga Imani – kuwa mwenye kuaminika

Mfanye mwenzio akuone wa kuaminika, usiwe muongo – mfano ukitoa ahadi jitahidi kuitekeleza hata kama si kwa muda muafaka aliotegemea.

Usimfanye akuone mbabaishaji na mjanja mjanja asieyeaminika.

Thamini hisia za mwenzako

Usipuuzie hisia zake – jaribu kushughulikia mambo ambayo mpenzi wako anayapenda.

Yawezekana mapendeleo ya mpenzi wako si sawa na yale ambayo wewe unayopenda.

Kwa mfano, mwenzako anapenda filamu za kikorea ilhali wewe unapenda filamu za Hollywood, basi jitahidi kuweka uwiano katika mapendeleo/interests zenu.

Kuwa msikilizaji mzuri

Jifunze kuwa msikilizaji mzuri – msikilize ili ugundue ndani mwake anawaza nini, msikilize na jitahidi kufanyia kazi anayokushauri.

Wakati mwingine unaweza kuona mwenzako hakushirikishi mambo yanayomhusu – anafanya hivyo kasababu anajua hata akikuambia huwa hausikilizi
hivyo anaamua kuyaweka moyoni mwake tu.

Ongeza mbinu za kutatua migogoro

Katika mahusiano migogoro haiepukiki – hivyo unatakiwa kuwa na mbinu za kuweza kuitatua migogoro hiyo, mwenzako akinuna jaribu kuwa mbunifu kumfanya afurahi tena. Ni lazima uwe na nguvu ya kufuatilia na kutatua matatizo yote.

Makala hii imeandaliwa na Shukuru Amos, mmiliki wa kampuni ya Tanzlite.

Share Your Thoughts With Me

Translate »