Nina tips chache za kushare kwenye hii topic, ambazo huwa ninazitumia ninapotaka kupata marafiki wapya.

Kuna kipindi wakati namaliza chuo, marafiki zangu wengi walikuwa wamesafiri na wengine walikuwa mikoani hivyo nikatamani kutengeneza marafiki wapya…. Nilizitumia tips hizi..

Labda tu niseme ni tips za jinsi ya kupata marafiki kwenye maisha ya kawaida/ in real life na sio kwenye mitandao ya kijamii.. Sasa kama unatamani kupata followers wengi mitandao ya kijamii na unatamani kujua jinsi ya kupata followers Instagram au mitandao ya kijamii mingine hii posti haihusiani na hivyo.. In fact Mimi pia situmii mitandao ya kijamii, siwezi kukusaidia hapo.

Twende moja kwa moja kwenye tips sasa:

Ujitoe kuwa wa kwanza

Unapotaka kupata marafiki usisubiri ufuatwe.. Unaweza kuwa wa kwanza kuwafuata.. Unaweza ukawa kimbelembele kuwaongelesha, kuwabebea mizigo, kuwapigia kwanza, kuwa text… Be persistent

Fanya vitu unavyopenda kuvifanya

Ili kupata marafiki mnaoendana, Fanya vitu unavyopenda kuvifanya.. Wale watu utakaokutana nao huko kuna chance kubwa sana ya nyinyi kuwa marafiki wazuri kwasababu mnashare vitu sawa. Kwahiyo kama ni michezo, jiunge kwenye timu ya michezo, wachezaji wenzio wanaweza kuwa marafiki zako, kama ni kuimba pia hivyo hivyo.

Waalike kwenye matukio au kubali ukialikwa

Ili kujuana zaidi ni vizuri kuspend muda pamoja, hivyo waalike marafiki zako kwenye lunch, kwenda out pamoja au pia ukialikwa jitahidi kukubali na kuhudhuria ulipoalikwa… Ili tu mspend muda pamoja upate kumjua huyo rafiki yako kwa undani.

Jitahidi kuonesha muonekano wa kwanza mzuri
Kama unatafuta marafiki, kila saa uwe kama mtu anayetafuta marafiki.. Kuwa approachable, open minded na on the look out kwaajili ya marafiki kila utakapokuwa.

Lakini pia uwe open minded, unaweza ukakuta mtu akuwa vizuri kwa wakti huo akakuonesha picha mbaya kuhusu we we, ila baadae ukaja kumjua vizuri na kujua ni mtu wa tofauti..

Jitahidi kuuliza maswali

Njia mojawapo ya kumjua mtu ni kuuliza maswali. Lakini pia wewe kujieleza.. Uliza maswali lakini pia elezea nia yako ya kutaka kumjua huyo rafiki.

Be Yourself

Ili kupata rafiki atakayekupenda vile wewe ulivyo, be yourself.. Usiigize kuwa mtu ambaye wewe sio.. Usiigize kufanya vitu ambavyo hauvipendi ili tu upate marafiki, utachoka kuigiza. Just be yourself, utapata watu watakaokupenda vile ulivyo.

Ila pia naomba niseme, kuna kubembeleza urafiki ambao kabisa unaonekana hautakiwi kuwepo, sio lazima kulazimisha marafiki hasa kama unaona hamuendani, au unaona ni mtu ayekupeleka muelekeo ambao we we hautaki kwenye maisha yako,au kama yeye anaonekana hayuko interested kuwa rafiki yako.

Sio lazima kulazimisha urafiki, inabidi uchague marafiki kwa hekima pia, ila pia wale wanaopenda kuwa marafiki zako.

Hizo ndio tips zilizonisaidia kupata marafiki.. Natumaini zitakusaidia na we we.

Eunice

You May Also Like

11 thoughts on “Jinsi ya kupata marafiki | 6 Tips

 1. Rabieth pascal

  Niceee and interested

  1. Eunice Tossy

   Asante sana Rabieth!!

  2. Eunice Tossy

   Thank you so much for reading!

   1. @bokerr

    Mafunzo yako mazuri na nimeyapenda sana naomba uongoze juhudi utafika mbali sana.

    1. Eunice Tossy

     Oh asante sana Bokerr.. Nimefurahi kusikia hivyo

    2. Eunice Tossy

     Asante pia kwa kusoma Bokerr

 2. Mambo ya kufanya unaposalitiwa na mpenzi wako – Eunice Tossy

  […] Unaweza pia ukamshirikisha rafiki yako wa karibu, wa kweli, ili awe nawe kipindi hiki kigumu. […]

 3. Maisha ya Mbeya kwa wanachuo na jinsi ya kufurahia kusoma mkoa huo – Eunice Tossy

  […] Soma Makala Hii : Njia 6 za kupata marafiki […]

 4. Sababu 6 zinazowafanya watu wengi wafeli kwenye maisha – Eunice Tossy

  […] Je marafiki zako wanakuongozea au kukupunguzia? Katika malengo yako wanakusukuma kwenda mbele au kukurudisha nyuma? Je marafiki zako wanakusaidia kukua katika maisha auhawakusaidii chochote? Kuna muda itabidi uache marafiki fulani fulani kwasababu unapoelekea kwenye maisha hauwezi fika kwas… […]

 5. Joseph Majura

  Thanks, sis Eunice and God bless you ………and bila kumsahau leo nashukuru nimelipatia jina lako am proud this improvement

  1. Eunice Tossy

   ha ha! nimefurahi pia umelipatia, hongera sana kwa improvement hiyo

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป