Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku

Kushindana kwenye maisha na jinsi inavyoathiri maisha yetu

Mashindano kwenye maisha..

Kwenye masomo, kwenye kazi, kwenye Mali tulizonazo, kwenye mavazi, hata kwenye mitandao ya kijamii.

Nakumbuka kuna siku nilisoma kwenye Twitter, na kuna mtu alimpongeza kijana mmija kwa kuanzisha kitu, na akamwambia kuwa, ‘this is really, in this world full of competition and challenges, this will be really helpful to young people’.

Nilisoma ule ujumbe na kujisikia vibaya. Mi napenda challenges, lakini sipendi mashindano. Naamini mashindano yanatutoa kwenye kusudi kuu LA maisha. Na hayana msingi.

Kuna watu huamini mashindano yanakupush na kukufanya uwe bora zaidi, kwahilo nawaza, je kweli ulikuwa unania ya kuwa bora zaidi kwa ajili yako, au unatamani kuwa bora ili umpite huyo unayesema ameku’push’?

Soma : What to do when you are struggling with comparison and envy

Tunaanzaga kufundishwa mashindano mapema sana, kiasi kwamba ndio tunahisi ndivyo maisha yanatakiwa kuwa, toka utotoni unaambiwa, ‘yani huyu kachelewa kutembea kuliko wenzake’.

Au ukiwa shule utakuwa unashindana ili uwe wa kwanza, kuliko wote.

Naona kama inabidi tuangalie na kuuliza maswali kuhusu vitu Vingi vilivyopo kwenye system, kwasababu japokuwa ni vizuri, vinaweza kuwa vinatuaffect kwa namna moja au nyingine.

Mimi ni shangazi, na binamu yangu Miry, amerudi Jana na mitihani yake ya chekechea. Uzuri ni kwamba mwalimu hakuandika amekuwa wangapi, Ila Miriam alikuwa anatuambia amekuwa wa kwanza. Akiwa na miaka 5 tayari anajali nafasi aliyopo ukilinganisha na darasa lake, tayari anahisi kuwa wa kwanza kunamfanya awe bora na kuwa wa thamani.

Soma : Ukiangalia maisha ya wengine, ya kwako yanakupita

—Mashindano yanatufanya kukosa urafiki wa kweli na watu, kwasababu hatuwezi kuwa wa kweli kwao, hatutaki kuwa chini yao au wao chini yetu, hivyo tunakuwa na urafiki superficial, urafiki fake.

— Mashindano yanatufanya kutoishi maisha huru, maisha ambayo yanajua kua kila mtu anasafari yake kwenye maisha, maisha ya huzuni na wivu wenzetu wakifanya bora, maisha ambayo kila siku unaona hauko enough, maisha tunayoona uthamani kutokana na sehemu tuliyonayo au nafasi tuliyonayo ukilinganisha na wengine.

— Maisha ya mashindano yanatupa stress, kwa vile tunaona kila siku tutashindwa au kuna mtu atachukua nafasi yetu.

— Maisha ya mashindano yanatufanya kuwa na roho mbaya na kushindwa kusaidia wengine. Kufurahia wengine wanaposhindwa na kuishi kwa kuwatumia watu ili tufike sehemu tunayohisi tutakuwa juu yao.

Tunaweza dhani kuwa hivyo ndivyo maisha yalivyo, ila Mimi naamini sana kwenye Uhuru na amani ya moyo, na kushindana hakuleti vitu hivyo. Cha zaidi yanatufanya tujisikie tuko nyuma kila siku ukilinganisha na wao walivyotupita.

Soma: Kama unahisi maisha yako yanaenda taratibu kuliko wengine

Kila mtu anasafari yake ya maisha, natamani sana niishi yangu na kufurahia wakati naiishi.

Anza kwa kujiuliza umejifunza yapi kuhusu maisha wakati unakua, na jiulize kama hivyo ndivyo unatamani kuishi, unaweza kuchagua jinsi unataka kuishi kwasababu maisha ni yako.

Pia kila unapojiona unashindana kwenye lolote kwenye maisha, jiongeleshe mwenyewe na kujikumbusha vile umeamua kuishi, halafu rudi kwenye mstari wako uliochagua.

Eunice

Translate ยป