Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Maisha ya kila siku

Maswali 4 ya kujiuliza unapofikiria kurudiana na mpenzi wako mlioachana

Muda mwingine kwenye maisha unajikuta upo kwenye hali ambayo unajisikia kurudiana na mpenzi wako au uhusiano wenu uko complicated kiasi kwamba inawezekana haujui uhusiano wenu umeisha au unaendelea, huwa inatokea.

Pia Soma : Mambo yakufanya unaposalitiwa na mpenzi wako

Kama umejikuta katika njia panda ya kutokujua kuwa umrudie mpenzi wako au lah, ningependa kushea na wewe maswali ambayo inabidi ujiulize kabla ya kufanya uamuzi huo, maswali yenyewe ni;

Je unamrudia kuepuka upweke au unamrudia kwasababu ya woga?

Kuna sababu nyingi zinazowafanya watu wawe kwenye mahusiano, wengine huwa kwenye mahusiano kwasababu ya upendo, wengine huwa wapo kwasababu ya kujisikia upweke, na kwa kesi hii ya kuwa mliachana hapo kabla inawezekana ukawa ni woga wa kuhisi kuwa huwezi pata mtu mwingine, inawezekana ikawa unajisikia vibaya kwasababu ya vitu ulivyowahi kumfanyia (hatia), kuwa singo muda mwingine kunakufanya ujihisi uko peke yako na hivyo unaweza jisikia vibaya kuwa hivyo au unaweza kujisikia upweke na hiyo pia inaweza kuwa sababu. Je unamrudia kwasababu gani haswa?

Je amebadilika yale aliyoyafanya na yaliyokufanya umuache

Kiufupi : Sababu iliyokufanya uachane naye mara ya kwanza haipo tena?

Wakati ulipoamua kuachana naye wakati ule kulikuwa na sababu nzuri sana za kuachana, je hizo sababu unazichukuliaje sasa hivi? Na je kama zilikuwa zinahitaji mabadiliko au maongezi, umeyaona au mmeongea kwa uwazi? Mara nyingi huwa tunapotezea na kuhisi jinsi ulivyoona hali mara ya kwanza tulikosea lakini baada ya muda unajihakikishia kuwa kumbe hata uamuzi ulioufanya kwanza ulikuwa sahihi au hali inajirudia kama ilivyokuwa mara ya kwanza. Hakikisha kuna mabadiliko unayoyahitaji.

Je mahusiano yenu yataonekanaje / yatakuwa na mabadiliko gani baada ya kurudiana?

Hili linaendana na hilo swali la hapo juu, uhusiano wenu utakuwa katika muonekano upi au utakuwa una mabadiliko gani ili msiangukie shimo mliloangukia mwanzo?

Je moyo wako una amani na uamuzi huo au unasitasita?

Ni vizuri kusikiliza watu ila pia ni vizuri kujisikiliza. Mahusiano yako tofauti kwahiyo sio kila ushauri unafanya kazi kwa wote Sikiliza moyo wako, sikiliza hisia zako unapofikiria hili swala, sikiliza sauti yako ya ndani. Huu ni uamuzi wako, unajisikiaje unapoufanya?

Pia Soma : Mambo ya kuzingatia unapopokea ushauri

Mwisho wa siku wewe ndio utaishi na maamuzi yako, kwahiyo hakikisha wewe ndio unafanya uamuzi wako na hakikisha unakuwa na amani ya moyo unapofanya uamuzi wako.

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »