Nimepata hii idea kutoka kwa Jessica, na alikuwa anaposti kwenye status yake, nikaona ni kitu kizuri sana namimi niandikie blog post.

Mwaka huo unaisha, naona kama mwaka ulianza juzi tu lakini tayari ni November, na mwaka mpya ndio unakaribia mlangoni ukiwa tayari kuingia.

Nimefikiria tujiulize maswali ili tuangalie tumeishije mwaka huu, eneo gani tuongeze bidii mwaka ujao, eneo gani tumejivunia sana jinsi tulivyoishi nk.

Maswali yenyewe ni:

1. Kitu gani umejifunza kuhusu maisha katika mwaka huu?

2. Kitu gani umejifunza kuhusu wewe ndani ya mwaka huu?

3. Ni mpango gani uliouweka katika mwanzo wa mwaka na haujautimiza?

4. Mipango ipi umeitimiza?

5. Vitu gani ungetamani ubadilishe kuhusu jinsi ulivyoishi mwaka huu?

6. Kitu/vitu gani vimekufanya ushindwe kutimiza malengo uliyopanga?

Pia Soma : Kwanini siamini kwenye kuweka malengo ya mwaka mpya

7.Na umejiandaaje kuvikabili katika mwaka ujao?

8. Umejifunza skill gani mpya mwaka huu?

9. Ongelea ukuaji wako katika mwaka huu kama binadamu.. Katika maeneo ya hisia, uchumi, elimu, kimwili, kiroho nk.

10. Ukiambiwa uelezee mwaka huu ulivyokuwa kwako kwa neno moja, utasema ni lipi?

La nyongeza…

11. Kitu/ vitu gani umetimiza katika mwaka huu ambavyo vinakufanya ujivunie?

Eunice

You May Also Like

2 thoughts on “Maswali 10 ya kujiuliza tunapoelekea mwisho wa mwaka

  1. Kwanini siamini kwenye kuweka malengo ya mwaka mpya - Eunice Tossy

    […] pia mwisho wa mwaka huwa nafanyaga ukaguzi wangu, kujikagua jinsi nilivyokua, wapi natamani kujiona naenda na kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita, […]

  2. Kwanini siamini kwenye kuweka malengo ya mwaka mpya – Eunice Tossy

    […] pia mwisho wa mwaka huwa nafanyaga ukaguzi wangu, kujikagua jinsi nilivyokua, wapi natamani kujiona naenda na kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita, […]

Share Your Thoughts With Me

Translate »