Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Vitu vya kufanya ili ufanye field vizuri na upate A

(Bonyeza hapa kusoma makala mbalimbali za mambo yote kuhusu Maisha ya Chuo)


Mara nyingi field huwa na credit kubwa sana, yani kubwa mpaka inaweza kukusaidia kukubadilishia na kukuongezea GPA.Mbali na kuwa unapata mafunzo ambayo yanaweza kukusaidia baadae, na kuwa field ndio sehemu zako za kwanza za kazi ambazo utaziweka kwenye CV, kupata A kwenye field kunakusaidia sasa hivi kwenye GPA lakini pia kuacha mahusiano mazuri na sehemu uliyofanya field ni muhimu kwani hauwezi jua unaweza ukapata reference au sehemu ya internship ukimaliza chuo.

Sasa hizi hapa ni namna mbalimbali zitakazokusaidia kufanya field vizuri, kumaliza vizuri na hata kupata A:


1. Usidoji, au ukidoji mtaarifu anayekusimamia field maana atakuja kukusainia kazi uliyofanya. Lakini pia hakikisha unawahi jamani.2. Andika ripoti kila wikiendi, ili usisahau yale uliyoyafanya kila wiki, na pia unakuwa unaandika taratibu sio kwa presha kama ukitaka kuzima moto mwisho wa field au supervisor anapokaribia kuja

3. Hakikisha siku ambayo masupervisor wanakuja haukosi kuwepo, ukikosa halafu watu wakakupigia simu sio vizuri.4. Jitahidi kufanya kazi unazopewa kwa lengo la kujifunzana kwa uwezo wako wote ili pia uonekane unachofanya. Jitoe na uwe unamaliza kazi mapema.5. Jitahidi kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wengine. Japokuwa ni kwa muda mfupi ila wewe pia ni sehemu ya ofisi, jishushe ili ujifunze. Jifunze kwa kila mtu. Usifike ukawadharau wafanya usafi au technicians kwa vile wewe unasomea kozi ambayo inaweza kukufanya wewe bosi wao, jishushe, kula wanapokula, sikiliza stori zao, mafundisho yao, utajifunza mengi kuhusu kozi, kazi na maisha.6. Kwenye daftari la ripoti, chora michoro mizuri, ukichora mwenyewe ni vizuri sana kuliko ukiprint halafu ukabandika.

7. Fanya kazi inayoonekana ili yule anayesaini ripoti yako pale field akusainie vizuri, huo ndio wepesi wa kupata A8. Lakini pia daftari la ripoti lijaze kwa ustadi, pangilia notes vizuri.9. Shirikiana na wanafunzi wenzio hata wavyuo vingine. Unaweza pata marafiki wapya lakini pia unaweza pata notes za kujazia kwenye daftari lako la field10. Usichelewe kuanza field, na usimalize pale tu utakaposainiwa na supervisor, fanya muda wote uliopangiwa na chuo. Ukionyesha ustadi mzuri pia sehemu unahofanya field wataona kazi yako, lakini pia wewe utajifunza mengi kuhusu kozi unayosoma.


Ni rahisi sana kupata A field, ila jambo likiwa rahisi ndio huwa tunalidharau na kuhisi tunaweza kulipata kiurahisi bila kujituma.

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate »