Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

Maisha ya kila siku Random
Eunice Tossy  

Faida na Hasara za kuishi nje ya mji

Nakumbuka siku tumetoka mkeshani, tukawa tunatembea kwenda kutafuta basi alfajiri, watu wakaanza ulizana, ‘wewe unakaa wapi?’.

Kila mtu akitafuta nani anaenda naye safari moja.

Kuna mmoja akaniuliza nikamtajia, akasema, ‘kumbe kule kijijini?’

🙄

Naishi Dar lakini.

Ila kuna sehemu tumeziweka kuwa ni nje ya mji na nyingine ni ndani ya mji.

Nawaza ndani ya mji ni maeneo kama posta labda, kariakoo, makumbusho, maeneo ya mlimani labda, na mengine naomba unitajie kwenye comment.

Nje ya mji itakuwa Mbagala kwa mbele, Kimara kwa mbele, kigamboni kwa mbele, na maeneo mengine ambayo naomba unitajie kwenye comment.

Zamani walikuwa wanasema sehemu yoyote inayochukua mabasi mawili kwenda sehemu nyingine ni nje ya mji🤣🤣🤣..

Ila Dar kubwa jamani. Kubwa sana.

Basi baada ya kukaa ‘nje ya mji’ kwa miaka saba sasa toka tuhamie huku, hizi hapa ndio faida na hasara ninazoziona:


Hasara

Watu wanapaita kijijini

Sina shida na neno kijijini maana ni neno ambalo tumelikariri kuelezea sehemu yoyote ambayo tunahisi haijaendelea, ila tu huwa nawaza kuna kijijini hapa na kijijini mikoani nabaki tu kuchanganyikiwa.

Usafiri shida

Si utani. Yani kwa vile bado miundombinu haiko poa basi mabasi ni shida/machache. Halafu kuna watu wengi kibao tunaokaa huku ila basi tu🙈🙈

Miundo mbinu bado haipo vizuri

Barabara hazijajengwa vizuri sehemu nyingine, maji ya kisima sehemu nyingine nakumbuka haswa tulivyokuwa tunahamia sasa hivi kuna bomba, umeme unakuwa haujafika sehemu nyingine inabidi uite TANESCO uanze moja nk.

Majirani wanaweza kuwa wachache na inabidi utengeneze marafiki wapya

Watu wanaweza wakawa bado hawajaamia, watu wako radhi wakae ‘mjini’ na joto lote hilo kuliko wajenge ‘nje ya mji’.

Aibu inayotokana na kukaa maeneo fulani

Niliandika kwenye hii makala, jinsi gani nilipata shida sana siku za kwanza tulipohamia Mbagala.

Watu wengi wanavile wanafikiria kuhusu eneo fulani na kuna namna tunaheshimu/tunadharau watu wanaokaa sehemu fulani, kuna namna tunaweka picha na kufikiria maisha ya wanaokaa sehemu fulani kiutofauti, hivyo kuna ile aibu au kuongelea kwa kutokujisikia vizuri kuhusu kule unapokaa.


Faida

Chakula bei rahisi

Huku kwetu kuna mashamba kabisa🤣🤣🤣

Hali ya hewa nzuri

Sanaaaa, yani usiku hadi baridi. Nakumbuka kabla hatujahamia huku tulikuwa tunagombania feni🤣🤣🤣

Ukimya

Huku kumetulia kiukweli, hakuna kelele, vigodoro🤣🤣🤣🤣 nk

Viwanja bei rahisi

Hata ukipanga chumba bei rahisi sana yani hela unayolipa ni sawa na bure🙄🙈🙈🙈

Bado kuna eneo kubwa hata ukinunua viwanja, sio kama ‘mjini’.

Kuna fursa nyingi

Za kilimo, uongozi, biashara nk. Kwavile bado mji unakua, fursa za mambo ya kufanya ya maendeleo ni nyingi.


Na hizo ndio faida na hasara ninazoziona mimi za kukaa nje ya mji.

Vipi wewe unaona faida/hasara zipi za kukaa nje ya mji?

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »