Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Career Guide,  Dondoo za Maisha

Jinsi ya kuwa na matumizi mazuri ya hela

Likija kwenye swala la hela, ni swala linalomuhusu mtu binafsi na ndio maana huwa sipendi sana kuandikia kuhusu swala hili.. Lakini kuna mmoja wetu kwenye comments aliniambia anatamani kujua jinsi ya kutumia hela anayoipata kwenye mshahara, na hivyo nikaona sio vibaya kutoa mawazo yangu kuhusu hii topic.

Uzuri wa hela hasa ambayo inaingia kwa mshahara ni kwamba ipo constant, mwisho wa mwezi lazima uipate.

Na hivyo unaweza kufanya vingi, ukijua mwisho wa mwezi utaipata tena.

Na ubaya wa hela ya hivyo, ni kwamba ipo constant, mwiaho wa mwezi lazima uipate.

Na hivyo tunatumia bila kujipanga tukijua kuwa mwisho wa mwezi lazima uipate.

Lakini kwa miaka minne niliyokuwa napata boom, na huu mwaka mmoja mtaani nimejifunza mambo machache kuhusu hela, na mengine nimeambiwa na wengine.

So nashara niliyojifunza na niliyoambiwa na wengine:

1. Kuandika mapato na matumizi kwenye Money manager app

Ili kukeep track ya pesa ninazozipata na jinsi ninavyozitumia huwa natumia money manager app. Hii inanisaidia kujua wapi ninapoteza hela. Na kiukweli ukiona hela umeiandika chini, kutumia vibaya ni ngumu sana kwasababu unajisikia uchungu fulani, lakini pia unaona thamani yake ya kuwa hela uliyonayo ni kubwa, na hivyo unaanza kuipangilia vizuri.

2. Kuandika vitu ninavyotamani kuvifanya kwenye mwezi

Ubaya wa hela ni kuwa hakuna hata siku moja inakosa matumizi.. Hivyo ukiipata kama unajambo ulitamani kulifanya ni bora ulivunje katika vitu unaweza kuvifanya kidogo kidogo.. Ila kusubiri hela kubwa ili itimie ndo ufanye jambo inakuwaga ngumu sana, lakini unaweza kufanya madogo madogo mengi. Hivyo kuvunja mipango yako kuwa mipango midogo midogo na kuanza kuifanya hiyo.. Kila mwezi unajua sh fulani nitaitumia kufanya jambo fulani linalonipelekea kwenye lengo fulani. Huu ushauri nilipewa na Goodluck Mkwizu.

3. Kuwa na kiwango unasave kila mwezi

Kwa usalama tu ili isije siku ukaishiwa kabisa au ukapata emergency halafu ukawa hauna hata hela ya kuanzia, ni vizuri ukiweka kiwango fulani kila mwezi kama akiba.

Inaweza ikawa hata 20,000/= ukiiweka kila mwezi inakuwa kubwa.. Hiyo hauigusi kabisa, inakaa tu.. Akiba ya chochote unachotamani kufanya. Na honestly kama unakuwa mwaminifu kutokuifanyia chochote unaweza ukasave ukafanya kitu kikubwa.. Au hata ukafanya kitu ambacho kikawa kumbukumbu ya kuwa ulishawahi kuwa na kazi fulani na umefanya kitu fulani kutokana na kazi hiyo.

Ushauri huu nilipewa na my mentor Caroline Nyagawa.

4. Usilete peer pressure ikuongoze kwenye matumizi yako ya pesa

Hela unayoipata ni yako, iwekee mipango yako. Hasa maofisini /vyuoni kuna mipango mingi sana ambayo unaweza kuiavoid kwasababu unajua unatamani ufanye kitu gani na hela yako. Hakikisha tu matumizi yoyote ya hela yako ni Yale uliyoamua na hautojisikia vibaya kuyafanya kwaajili yako. Jua kuwa maisha yako ndio yameanza, unaweza kutimiza ndoto zako, na pangilia kufanya hivyo.


Zaidi ya hapo kuna maswali ambayo unaweza kujiuliza ili kujiwekea matumizi mazuri ya hela yako:

— What do you want to do with your money?

(Unataka kufanya nini na hela yako?)

—How long do you want to stay in your job?

(Unataka kuifanya hii kazi kwa muda gani/au utaendelea kuipata hii hela kwa muda gani?)

—What are your goals?

(Una malengo gani?)

—What season are you in now?

(Upo kwenye majira gani sasa hivi kwenye maisha yako?)

—What are your dreams and plans? Which can be achieved using the money that you get

(Ndoto zipi na mipango ipi uliyonayo inategemea hela ili kutimia?)

— What are your plans for this year?

(Una mipango gani unayitaka kuitimiza mwaka huu)

—Where do you see yourself in 5 years and how can your current salary contribute to that?

(Unajiona wapi miaka mitano ijayo, na mshahara wako unachangiaje hayo maono?)

—What do you need now (make a list and tick it off slowly)

(Sasa hivi unahitaji nini?)

—How much do you make per year? (Hela inaonekana ndogo monthly ila yearly ni kubwa sana.)

(Mshahara wako kwa mwaka ni kiasi gani?)


If you want to do something big save, because if you wait for one big amount to come it never will or you will have a different use with it.

Na hayo ndio ninayoyajua sasa kuhusu matumizi mazuri ya hela.. I hope it is useful

Eunice

10 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป