Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Imani,  Maisha ya kila siku,  Random

Mwanamke sio jaribu

Nahisi toka Hawa ampe Adam tunda tumeweka kuwa wanawake ndio wasababishi wa dhambi, hata unayoifanya kwa mikono yako pia.

Kwenye familia, wanawake hulaumiwa mtoto akikuwa na tabia mbaya, nk.

Na sasa mwanamke analaumiwa hata akibakwa.

Alivaa nguo gani, kwanini alitembea usiku, kwanini hiki kwanini kile.

Mwanamke ndio chanzo cha magumu na mabaya yanayompata.

Mwanamke ndio mwenye jukumu la kuepusha mabaya yote, ikiwemo tamaa ya mwanaume.

Vaa nguo ndefu usionyeshe mapaja.

Mwanaume atakutamani.

Kaa staili fulani.

Makanisani usikae na wanaume, kila mmoja akae upande wake.

Nimekulia kanisa ambalo kuna sehemu ya wanawake kukaa na wanaume na kuna sehemu ya mchanganyiko, unachagua unakaa wapi. Pia kuna wengine wananguo zao za kuvaa, urefu fulani usipofika usiingie kanisani. Kwasababu wanaume wakikimuona wataanguka dhambini.

Na kubwa kuliko urafiki kati ya wanaume na wanawake unaangaliwa kwa jicho la tatu. Na haushauriwi na wengi maana kuwa rafiki yake kunaweza kukujaribu wewe mwanaume kuzini naye.

Wanawake wana jukumu la kumuepusha mwanaume asifanye dhambi. Dhambi ya uzinzi.

Jukumu ambalo jamii imewapa, na ambalo wanashindwa kulitimiza kwasababu ni jukumu la mwanaume mwenyewe.

Marko 9:47

Yesu alisema ng’oa jicho lako sio umlazimishe fulani akuzuie wewe kufanya dhambi.

Kuna case nyingi za wanaume wamebaka wanawake waliovaa madela, hijabu na watoto wa miezi tu waliovaa nepi, hii sio ishu ya mwanamke ndio msababishaji, hii ni ishu ya dhambi ya moyo ya mwanaume, na anatakiwa ‘ang’oe jicho lake yeye’.

Wanawake sio majaribu, unless unadeal na ishu yako mwenyewe ya moyo na dhambi fulani usimlaumu mwanamke

Kuna rafiki yangu mmoja wa kiume ambaye alikuwa anashida ya addiction ya picha na vedio za ngono, alinisimulia siku ambayo alikuwa anakula mgahawani na mdada akaingia amevaa kimini, alipomuona ilitrigger ile addiction yake na yeye akaona ni bora aondoke maana hali ilimbadilikia.

Siku niliposikia hii stori ndipo nilipoelewa kuwa dhambi ni jambo binafsi, ishu ya moyo, ya nje ni ziada tu ila shida ya moyo unakuwa nayo mwenyewe.

Tamaa ni personal na sio mtu alivyovaa na ndio maana hata masister wanabakwa.

Kila kitu tunakiangalia kwa jicho linalowaza ngono na ndio maana kila kitu kinaongelewa na kukatazwa kwaajili ya kuepusha ngono.

Lakini kwanini tusiwe na mawazo yaliyosafi? Ya kujua kuwa Mungu ametuumba tuwe dada na kaka, kuwaangalia wanawake kama binadamu, watoto wa Mungu wenye ufahamu na maarifa na ambao Mungu anaongea nao pia kwaajili ya maisha yetu kuliko kuwaangalia tu kama miili na chanzo cha wanaume na chakutamaniwa ambacho kitatufanya tutende dhambi tukikisogelea.

Kwanini tusiwe na mipaka ya mioyo yetu binafsi, tukienenda kwa hekima na akili.

Kwanini tunashusha hadhi uumbaji wa Mungu na kuufanya kuwa chombo cha starehe?

Kwanini tunapoteza kusudi la Mungu kutuumba kama kaka na dada hata makanisani?

Tunapoteza nafasi ya kujifunza na kusikia kutoka kwa wanawake kwa njia ya urafiki?

Kwanini tunafundishwa kuwaona wanawake kama chanzo cha jaribu la wanaume kuzini?

Eunice

One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate »