Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Random

Kuoa na Kuolewa ni sehemu ya kutimiza kusudi lako

Nawashangaa wanaoumiza vichwa vyao kwamba nikitoka chuo nani atanioa/ nitamuoa nani?

Mwanamke hukuzaliwa ili uolewe.
Mwanaume hukuzaliwa ili uoe.

Kuolewa au Kuoa ni nyongeza

Ulizaliwa kutimiza KUSUDI fulani soma Biblia Adam alipewa kazi kwanza bustani ya Edeni ndipo akapewa msaidizi!!!

“Mungu akaona si vyema Adam awe peke yake…”, msaidizi haji mzae watoto tu.

Dada acha kumsumbua Mungu akupe mume kama hujui ni nini umebeba ambacho kitaenda kusaidia kusudi lililo ndani ya mwanaume

Tafuta kujijua kwanza umebeba nini na kitamfaa nani?!

Pengine (binti) una tunu kubwa sana lakini ukiishia mahali ambapo haitumiki huo ndio mwisho wako.

Pengine (kijana) umeumbwa na hatima kubwa lakini usipopata mwanamke anayekufaa ukapoteza maono yako.

Una kitu gani?? cha kumsaidia nani???

Lazima ujue kwanini Mungu aliumba MWANADAMU kwanza, kuzaa/ kutengeneza familia ni sekondari … kuna kusudi lilifungwa ambalo ndilo litakaloamua yupi umalize nae mwendo.

Mwanaume umepewa kazi ya kwenda kutimiza vivyo hivyo mwanamke… ukienda tofauti na hapo lazima itakua ngumu/ yatakushinda

Hakuna kipimo cha uzuri vijana wa kiume… Je, ana kitu cha kukusaidia ???

Ndio kijana ni mtanashati lakini… Je, una kitu cha kumsaidia???

Nimepata sikia warembo walioachika, ndoa zenye migogoro na waliopoteza hatima zao… nikagundua kumbe uzuri hautoshi bali Kusudi la Mungu na Hekima ya kiMungu ndani ya huyu msaidizi.

Upendo ni Hisia
Uzuri nao unazoeleka na haudumu milele
Misingi yenu iko wapi??? Kuwa makini yasikushinde

Unaangalia nini kabla ya kuolewa/kuoa???


Imeandikwa na Christine Bellington

Mwandishi : Embrace Tanzanian Youth

Mchecki : Instagram na Facebook

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป