Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

african american couple having conflict at home
Dondoo za Maisha,  Guest Post

Njia 3 rahisi za kudhibiti hasira

Kama huna elimu juu ya hisia za binadamu utapata wakati mgumu sana kuishi na watu wengi. Utakwazana na kila mtu kwa kufikiri kuwa anawaza kama unavyofikiri wewe jambo ambalo si sahihi. Watu huongozwa na hisia katika maamuzi yao ya kila siku maana yake mtu akiwa na furaha atakusifia, atakushukuru, atakupongeza, atakuonyesha tabasamu. Akiwa na hasira atakuwa haionyeshi furaha yake, atakukosoa kwa ukali, atakufokea hata kwa vitu vidogo na atakukejeli.

Katika ubongo wa binadamu kuna prefrontal cortex ambayo ni sehemu ya ubongo inayofanya kazi ya kutatua matatizo makubwa sana, kutuliza hasira, kufanya maamuzi magumu, kufikiri juu ya maswali magumu. Pia kuna amygdala ni sehemu ya ubongo inayofanya kazi ya kupokea vichocheo vya hasira, vitisho, vitu vya kuogopesha, maumivu n.k.

Watu wenye hasira sehemu ya amygdala huwa inafanya kazi muda mwingi kuliko sehemu ya prefrontal cortex hivyo huongoza kwa kukurupuka, kutukana, kupigana, matusi, lawama, vilio, manung’uniko ya hapa na pale. Vitu ambavyo huchochea sehemu hiyo ya ubongo kuwa na hisia za hapa na pale ni mateso ya utotoni, kubaguliwa, ajali, kupitia unyanyasaji kama kubakwa, kubaguliwa, vipigo, kutumia pombe, bangi, vinywaji vyenye kuchochea hasira. Mtu ambaye huwa anapitia stress kama vile mahusiano mabaya, hali ngumu sana ya kiuchumi, kupelekeshwa kazini, kufanya kazi huku halipwi, kudhalilishwa, kuugua muda mrefu, migogoro ya kila siku, anayefanya kazi huku haipendi hupata tatizo la hisia kubadilika kila wakati na hasira za mara kwa mara.

Kuna aina mbili za stress ambapo kuna acute stress ambapo ni ile ya kawaida kama kuogopa kukutana na mtu mwenye heshima kubwa, kuogopa kuhutubia watu wengi, hofu ya interview, kuchelewa kazini, kuchelewesha kazi au kufika kwenye deadline kazi hujamaliza hizo ni za kawaida haziwezi kuleta msongo wa mawazo.

Ila chronic stress ni zile ambazo huwa zinakuja kwa mtu kuwa na mahusiano mabaya, ajali, vipigo, kufanya kazi asiyoipenda, kupelekeshwa kazini, kuugua muda mrefu, hali mbaya ya kiuchumi, kufilisika, kumpoteza umpendaye nk.

positive young african american lady holding light bulb in hand on gray background

Ikiwa unaishi na mtu mwenye hasira usipoteze muda kutaka uzitulize hasira zake huwezi na hutaweza. Hasira ni hisia ambazo huwa zinakuja na kuondoka ila ukiendelea kufikia vitu hasi kwa muda mrefu hasira itadumu kwa muda mrefu na kupelekea tatizo la msongo wa mawazo. Ukiona mtu ni mkali sana, anahasira sana tambua tatizo lipo kwake si kwako. Watu wengi wenye hasira ni tatizo la kiakili wala si makosa yako yanayomfanya awe hivyo. Mtu mwenye hasira za karibu ni wazi anatatizo la kiakili.

Pia Soma : Jinsi ya kujali afya yako ya akili

Sehemu ya ubongo inayofanya kazi ya kutatua matatizo magumu inayoitwa prefrontal cortex huwa inatuliza hasira, inashusha mapigo ya moyo hasa unapoogopa, ukiona mti usiku utafikiri ni nyoka kwa sababu amygdala hufanya maamuzi haraka ila prefrontal cortex huwa inatuliza hisia na kukufanya utambue kuwa si nyoka bali ni fimbo. Kwa mtu mwenye tatizo la kiakili prefrontal cortex huwa haifanyi kazi vizuri badala yake amygdala ndiyo humuongoza kwenye kila kitu kama maamuzi, kufikiri, tabia n.k. Mtu mwenye hasira sana hana akili timamu kwa sababu akili ni uwezo wa kufikiri unaomwezesha mtu kufikiria vitu kwa uhalisia.

Ikiwa unaishi na mtu mwenye hasira tambua kuwa anatatizo kwenye amygdala hivyo maamuzi yake yanakuwa yanaongozwa na mihemko badala ya prefrontal cortex. Watu wenye hekima sana,wapole, wacheshi sana, wenye kufikiri sana eneo la prefrontal cortex huwa tofauti na wale wenye hasira. Ubongo unafanya kazi ya kujiboresha wenyewe kila wakati maana kama ilivyo misuli ya mwili huwa imara unapofanya mazoezi na ubongo huwa imara unapofikiria sana mambo magumu. Ikiwa hufikirii matatizo magumu sana ubongo unalemaza na kuwa na uwezo mdogo sana wa kufikiri.

Pia Soma : Mambo matano yatakayokusaidia kudili na watu wagumu

Ukijizoesha kujifunza kila siku unabadilika umbile la ubongo na kukuwezesha kuyakabili maisha kwa upesi kuliko watu wazembe. Ikiwa utafanya mazoezi kila siku ya kufikiri sana utafanya prefrontal cortex ya ubongo kufanya kazi kuliko amygdala hivyo utajikuta huna hasira. Ikiwa itajitahidi kwa muda mrefu sana utaweza kuwa unahimili matatizo makubwa sana kuliko awali. Usikate tamaa kama unahasira sana na unakwazana sana na watu kwa sababu ya hasira. Kama utaamua kuanza kudhibiti hasira utakuwa mpole, mwelewa, mcheshi, mwenye furaha sana.

Furaha inasababishwa na hormones ndani ya mwili kama vile serotonin, oxytocin, dopamine homoni hizo huzalishwa pale unapotuliza akili. Akili ikitulia homoni hizo hufanya mwili kuwa katika utulivu na kukuwezesha kuona maisha katika uhalisia badala ya kuona mawenge.  Watu wenye hasira homoni zinazozalishwa kwa wingi ni cortisol ambapo homoni hizo humfanya mtu kuwa na mapigo ya moyo makali sana, kuvuta pumzi kwa kasi, kufikiri haraka na kupelekea kukosea kuliko mwanzo, humfanya mtu kukurupuka kwenye maamuzi, kuongea haraka bila kujua athari za maneno.
Madhara ya kushindwa kudhibiti hasira ni kukwazana na watu kila wakati, kupoteza dira, kukata tamaa, kujiua, kudhuru watu, kupiga, kutukana, kuvunja sheria, kupata madonda tumbo, kupata magonjwa ya moyo, uchovu, kujiweka hatarini kupata kisukari, kuchanganyikiwa, kukosa hamu ya kula, hedhi kuvurugika, kuugua mara kwa mara, kujitenga na familia, kupoteza kumbukumbu, kupata maumivu makali hata kwa vitu vidogo.

Furaha yako ni fikra zako.

Kumbuka unapoacha kujifunza unakwenda kuharibu ubongo wako mwenyewe.

Jipende sana na ujijali kuliko unavyoweza kumhudumia mgeni mwenye heshima anapokuja kukutembelea


Imeandikwa na Mwanasaikolojia – Said Kasege, Temeke, Dar es salaam

+255766862579, +255622414991

Share Your Thoughts With Me

Translate »