Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Self Care

Njia 3 rahisi za kuongeza thamani yako binafsi

Je unawaza ni jinsi gani unaweza kuongeza / kukuza thamani yako binafsi? Soma hii👇🏿


Kama kila kitu kingekuwa rahisi kupatikana basi, Kuna baadhi ya vitu vingekuwa havina thamani kabisa katika huu ulimwenguni, ebu jaribu kufikiria kuwa, kama dhahabu ingekuwa inapatikana barabarani tu , yani kila ukitembea unaiona, je ingekuwa na thamani??

Jibu ni hapana.

Sasa nataka kukuambia jambo moja, muhimu sana katika maisha yako..

Ebu jaribu kukuza thamani yako.

Na hizi ni njia tatu za jinsi unavyoweza kufanya hivyo;

Epuka kuishi bila ratiba

Jifunze kusema HAPANA sio kila ukiambiwa jambo unasema ndio.

Anza kusema HAPANA ili kulinda ratiba zako.

Mfano, twende canteen, aya twende, twende library, aya twende! twende mpirani, aya twende!

Ukiona mtu yupo hivi basi hana msimamo na maisha yake.

Pia Soma : Njia 5 rahisi za kujipenda zaidi mwaka huu

Kuwa na muda maalumu wa kuzungumza na nafsi yako.

Kumbuka sisi ni matokeo ya tunachokiwaza, sio kila muda unafikiria kuhusu wengine, ndugu yangu fikiri kuhusu wewe.. jitathimi ulikotoka na unakokwenda .

Punguza kuongea ovyo, ebu fanya maneno yako ni ya thamani sana, sio kila jambo wewe…

Siasa wewe, michezo wewe, burudani wewe.

Haya ni matumizi mabaya ya mdomo.

Kumbuka kuwa kukaa kimya ni dhahabu…kuwa na muda maalumu wa kuongea.

Pia Soma : Ukiwa busy kuangalia maisha ya wenzako, ya kwako yanakupita

Anza kutoa appointment

Sio kila mtu akikuhitaji unasema sawa, hapana anza kusema nitakuwa na muda Ijumaa.

Kama mtu huyo anajambo la kipuuzi lazima atapotezea lakini kama ni muhimu atakutafuta.

Hii inaongeza thamani yako…Na kuonekana upo makini na ratiba zako.

Jijari, jipende hii ni miongoni mwa safari nzuri za maendeleo..


Imeandikwa na Mr Yamungu Omary, ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akisomea Shahada ya Jinsia na Maendeleo. Pia ni mhamasishaji na Mwandishi wa kitabu cha” maendeleo ni wewe” na ni mwenyekiti wa taasisi ya ukombozi wa kijinsia kwa watoto.

Mawasilano – 0763855049

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป