Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

Dondoo za Maisha Self Care
Eunice Tossy  

Njia 5 rahisi za kujipenda mwaka huu / #selflove

Je unajipenda?

Chukua muda kujibu swali hilo…

Halafu tuendelee

Ni rahisi sana kuwapenda wengine, ni rahisi sana kuwaonesha upendo wengine kwa njia zinazoonekana kuliko kujipenda sisi wenyewe, moja kwasababu mtu ukiwa unajipenda unaitwa mbinafsi utasikia, ‘ jamaa ni mbinafsi sana yule, anajipenda sana’. Natamani niamini kuwa kuna namna inaweza kuwa ubinafsi ikiwa kama unajifaidisha wewe kuliko wengine hasa kwenye mazingira ambapo wote inabidi mpate, lakini mara nyingi woga wetu wa kuitwa au kuonekana kama wabinafsi unatufanya tusijioneshe upendo hata sisi wenyewe.

Mwaka 2021, weka malengo ya kubadilisha hilo maana hata vitabu vya dini vinasema wapende wengine kama unavyojipenda, na kwa vile ibada njema inaanzia nyumbani haisaidii wewe kwenda kilomita mia kuwaonesha wengine upendo wakati wewe mwenyewe umejitelekeza.

(Pia Soma : Kwanini siamini kwenye kuweka malengo ya mwaka mpya)

Kama nimekushawishi kuweka lengo hilo basi hizi ni namna tano rahisi za kujionesha upendo mwaka huu;

  • Kubadilisha vile unavyojiongelesha

Kuna maongezi mengi sana yanatokea vichwani mwetu ambao watu hawayasikii, je ushawahi kukaa kuwaza kuhusu maneno unayojiambia? Je unaweza kumwambia mtu unayempenda hayo maneno? Fanyia kazi kuyasikiliza ili uyabadilishe maana vile unavyojiambia, ndivyo utkavyokuwa unajiona. Ukijivunja moyo kichwani, utashindwa kujaribu, utakuwa unahisi hauna thamani, na utajawa na woga. Amua kujipenda kwa kubadilisha maneno unayojiambia, badilisha kujiongelea maneno hasi, kujiponda nk.

man in red polo shirt smiling
  • Jinunulie zawadi au jifanyie zaidi vitu unavyovipenda

Nimesema jinunulie zawadi kwasababu mimi napenda zawadi, kwahiyo kujinunulia zawadi kunanifanya nijisikie vizuri, nijisikie najipenda. Kuna furaha inayokuja ukimnunulia mtu kitu halafu akakipenda, kwanini usijipatie hiyo furaha wewe pia kwa kujiunulia kile unachokipenda? Na sio lazima kiwe kikubwa, unaweza hata kujinunulia tunda huku ukiweka nia ya kuwa unalinunua ili kujionesha upendo. Au kama kuna kitu ukikifanya unajisikia vizuri, unajisikia kama wewe Zaidi, fanya hayo kwa wingi mwaka huu. Yale unayoafanyia wale inaowapenda kama ndio yanayokufanya ujisikie kupendwa pia, jifanye na wewe, raha jipe mwenyewe.

Pia Soma : Jinsi ya kuukubali na kuupenda mwili wako vile ulivyo

  • Punguza matumizi ya vitu vinavyokuchosha

Inawezekana ni mimi tu ila nikitumia mitandao ya kijamii kwa muda mrefu huwa nachoka, nikifuatilia sana skendo za wasanii naanza kujisikia vibaya na kuchoka pia, yani kuna vitu ambavyo inaonekana ni kawaida kuvitumia au kuvifanya ila nimefika wakati naona kuwa havinifai tena kwaajili ya maendeleo yangu mwenyewe binafsi na kwa maisha ninayotaka kuishi.

Njia moja wapo ya kujionesha upendo ni kuishi katika namna inayokuletea wewe zaidi furaha, inayokufanya ujisikie kama wewe, inayokupa amani na furaha ya mooyo. Ni vitu gani ulikuwa unavifanya mwaka uliopita ambapo mwaka huu unatamani uviache kwaajili ya kuboresha maisha yako? Hiyo pia inaweza kuwa njia ya kujionesha upendo.

black girl with faceless friend on stadium
  • Pumzika

Chukua muda kupumzisha moyo, akili na nafsi. Mambo yanaenda haraka sana, unaweza kukimbia nayo ila kwa vile sisi ni binadamu kuna muda unafika tunachoka, unapochoka chukua muda kupumzika. Au andaa mfumo unaokusaidia kupata mapumziko kabla haujachoka, hii ni kujipenda pia.

  • Sema hapana unapojisikia kusema hapana

Kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kusema ndio na wakati wa kusema hapana. Mara nyingi hata kama tumechoka, au hatujisikii kufanya jambo fulani kutoka ndani huwa tunaogopa kusema hapana kwa vile hatupendi mtu fulani ajisikie vibaya au atufikirie vibaya. Hivyo tunasema ndio japokuwa mioyo yetu inasema hapana na hivyo tunajikatili sisi wenyewe ili kufurahisha wengine. Mwaka huu tujifunze kusema hapana, utajisikia vibaya mwanzoni lakini baadae utazoea kufuata amani yako ya moyo, na hiyo ni njia mojawapo pia ya kujionesha upendo kwa kuwa unaweka amani ya moyo wako mbele ambayo hii pia inakuletea furaha.

Najua una malengo mengi ya mwaka mpya ila nimetamani nikushirikishe haya ili kujipenda mwenyewe kuwe moja ya malengo yako, na njia hizi rahisi zitafanya lengo lako hili litimie kiurahisi.

Eunice

3 thoughts on “Njia 5 rahisi za kujipenda mwaka huu / #selflove

  1. […] Jifunze kusema HAPANA sio kila ukiambiwa jambo unasema ndio. […]

  2. […] mawazo chanya14. Kuwa mwenye Subrah (mstahimilivu)15. Fanya mazoezi16. Fanya tahajudi (meditate)17. Weka hitaji lako kuwa ni kipaumbele18. Epuka kuwa mtu wa visingizio19. Usiwaongelee watu kwa ubaya20. Sikiliza ili uelewe, Usisikilize […]

  3. […] Mi napenda kukimbia. Nahisi mazoezi yaliwekwa ili kila siku tuufanyishe mwili kazi, and so najaribu kuenjoy wakati nafanya mazoezi. Hivyo huwa napenda kukimbia wakati wa asubuhi ili nione sunrise au jioni nione sunset + nakuwa na music napumzika from time to time. Mazoezi sio lazima yawe mateso, you can even do dancing tu. Unajua tuna mwili mmoja tu hapa duniani ni muhimu kuujali lakini pia jitahidi kutafuta zoezi unalilo… […]

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »