Toka nilipokuwa high school nilikuwa najiuliza hili swali… Am I on the right path in my life?

Toka nikiwa shule nilikuwa natamani kujua kama course niliyoichagua haitonifaa kwenye maisha ili niiache, niende kwenye course sahihi..

Sikutaka kukosea kwenye maisha, nilitamani kuishi maisha sahihi, yasiyo na makosa, perfect.

Nikiwa chuo sana sana ndo nilijuliza sana..

Je, napoteza muda?

Je, hivi ndo nilivyochagua kwaajili ya maisha yangu?

Je, kuna kingine bora ambacho nakikosa kwasababu ya uchaguzi huu?

Vipi nikifika mwisho halafu nikagundua nilikosea kuchagua?

Maswali haya yalinifanya niumie, niogope kuishi maisha, yani niishi maisha kwa uangalifu mkubwa sana, ambao ni kitu kizuri na kibaya pia.

Nimefikia kipindi sasa hivi sijiulizi tena hili swali, lakini haikuwa rahisi..

Vile naona maisha sasa hivi, na vile nilivyokuwa naona maisha nikiwa high school ni tofauti..

High school nilikuwa naona maisha kama lengo, naishi ili nifikie sehemu Fulani. Nilikuwa naona kama mashindano, wenzangu wasifikie lengo, kabla yangu.

Soma : Kama unahisi maisha yako yanaenda taratibu

Sasa hivi naona kuishi ndio lengo, ni jinsi gani ninaweza kuwa na furaha wakati naishi, ni jinsi gani ninavyoweza kushwangazwa na maisha, kuishi katika wakati niliopo.. Siku hizi naishi kila siku kama inavyokuja, siku hizi naona maisha kwa jicho la tofauti.

Kuna vitu vimenisaidia kuishi hivyo na kunifanya kuacha kujiuliza hilo swali..

1.. Kujua kuwa Mungu anajua mwanzo na mwisho wa maisha yangu

Nilipojua kuwa maisha yangu yanavyotokea na yanavyoendelea kuwa sio surprise kwa Mungu, kwani yeye anajua mwanzo na mwisho niliona haiwezekani kuwa kwenye njia ambayo sio sahihi kwenye maisha yangu kwani hata njia ninayodhani sio sahihi, Mungu ameiruhusu niipitie.. Hivyo bado nipo kwenye njia sahihi kwenye mpango wa Mungu. Haitotokea hata siku moja nikaishi maisha au nikapita sehemu ambayo Mungu hajairuhusu, hata pale ninapoona nimekosea, au kuwa sio njia sahihi kwaajili ya maisha yangu.

2.. Kujua kuwa hakuna makosa kwenye maisha, kuna kuishi tu

Nimegundua kuwa tunaangalia maisha kama insha, lazima mpangilio ufuatiliwe, kuanzia utangulizi mpaka hitimisho.. Lakini Mara nyingi maisha hayapo hivyo. Hakuna makosa kwenye maisha, kuna kuishi. Tunaishi tu. Kwamfano kuna kipindi nilikuwa najiuliza kwanini Mungu aliruhusu nisome Mechanical Engineering ambayo kwasasa naona sina moyo wa kuifanyia kazi, lakini nikajikumbusha point hiyo ya kwanza. Nakugundua kwamba kama isingekuwa kwa miaka hiyo minne niliyospend chuo, nisingekuwa Mimi ambaye nipo sasa hivi, nisingegundua nini napenda kwenye maisha lakini pia bado naishi kwahiyo kwavile sasa nafikiri kitu kingine ndio ‘sahihi’ ninaweza kukisomea pia. Kwavile bado naishi, kuna second chance / kuishi tu.

Nafikiri tunapowaza sana kuhusu kama tuko njia sahihi, swali hili linatufanya tukose nguvu ya kujaribu mambo kwasababu tunaweza kuyaona sio sahihi, na hivyo kupoteza furaha katika kujaribu vitu mbalimbali kwenye maisha.

3.. Kujua kuwa maisha hayaendagi vile tunavyopanga

Maisha yanachekesha sana kwakweli.. Huwa hayaendagi vile tunadhani tumepanga yaende, tujikumbushe point ya kwanza. Mungu hutupitisha katika njia anayoona Yeye inatimiza kusudi lake kwenye maisha yetu.. Baada ya kujua hili nimepunguza sana mipango, nimeongeza sana kuomba mapenzi Yake yatimizwe kwenye maisha yangu. Kwahiyo hata tukipanga kutokuwa kwenye njia ambayo sio sahihi, inawezekana kwa Mungu hiyo ni sahihi kwa kusudi lake kwetu.

(Isipokuwa dhambi tu, sidhani kama inaweza kuwa ni kusudi lake tuwe kwenye njia ya dhambi, ila kazi, masomo nk, Mungu ni mwenye nguvu)

Jua tu, hauwezi jua vile maisha yako yanatakiwa yawe au yatokeaje, unachokifanya wewe nikuyaishi.

Eunice

You May Also Like

5 thoughts on “Je, nipo njia sahihi kwenye maisha yangu?

 1. Kwa waliochaguliwa course ambayo hawaipendi - Eunice Tossy

  […] nilikuwa sijui nahitaji nini kwenye maisha nikaona labda nitaipenda hii course na labda hii ndio njia ambayo nilipangiwa kwaajili ya maisha […]

 2. Kwa waliochaguliwa course ambayo hawaipendi – Eunice Tossy

  […] nilikuwa sijui nahitaji nini kwenye maisha nikaona labda nitaipenda hii course na labda hii ndio njia ambayo nilipangiwa kwaajili ya maisha […]

 3. Johnson

  Nabarikiwa sana na wewe, na najifunza mengi toka kwako kiukweli mimi ni mmoja wa watu ambao mpaka sasaivi nilikuwa nikijiuliza je nilichochagua ninsahihi au sio sahihi? Lkn napambana

  1. Eunice Tossy

   Naelewa unachomaanisha. Ni sehemu ngumu sana kujisikia hivyo aisee, nimeshapitia hapo. Hata kama haujachagua sahihi unaweza kubadilisha,kwavile maisha bado yanaendelea hakuna kitu ambacho ni mwisho, na haujachelewa.

 4. Sababu 6 zinazowafanya watu wengi wafeli kwenye maisha – Eunice Tossy

  […] Pia Soma : Jinsi ya kujua kama upo njia sahihi kwenye maisha yako […]

Share Your Thoughts With Me

Translate »