Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

architect architecture artist blur
Maisha ya Chuo

Mambo 5 ya kuzingatia unapochagua project ya kuifanya chuoni.

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Kozi nyingine hufanya mwaka wa mwisho, kozi nyingine hufanya miaka miwili. Mimi nilifanya miaka miwili, watatu na wanne. Naongelea project, na hivi huwa zina credit kubwa na ni alama ya kuwa umefika mwisho wa masomo yako, project ni module ya muhimu sana unapokuwa chuoni. Ili usichanganyikiwe ni namna gani utaipata project inayokufaa, ngoja nikupe mambo ya kuzingatia wakati unachagua project yako.

Mambo yenyewe ni haya yafuatayo:

1. Chagua title ambayo inatokana na vitu ulivyokuwa na interest navyo.

Itakuwa rahisi sana kuifanyia kazi project ambayo unainterest nayo kuliko vitu ambavyo hauna interest navyo kwenye course ambayo unaisomea, lakini pia vitu ulivyokuwa na interest navyo kidogo vitakuwa virahisi kwako lakini pia utakuwa una mwanga na direction kidogo kwenye hivyo vitu, kuliko kufanya kitu ambacho ni kipya kabisa. Kitu kipya kitakufundisha ila kitakucost either kukupa mawazo sana au pia kukufelisha.

2. Gharama ya project na utayari wako wa kuilipa

Kuliko kuingia kichwa kichwa kufanya project ambayo haujui cost yake in terms of muda, pesa, resources, contacts unazozihitaji kuikamilisha, ni bora ukakaa chini ukatafakari ni namna gani itakucost na utayari wako wa kulipa gharama hiyo.

3. Kitu unacho tamani kujifunza kutoka kwenye project yako

Project ni module ambayo wewe una power ya kuichagua at your own expense. Sasa unaweza kuwa unakitu unapenda kujifunza kenye area fulani ya course as costful as this is for non-risk takers, project inaweza kukupa uwezo wa kuwa mjuzi katika eneo fulani, kwa mfano most of my friends walifanya projects za kudesign vitu mbalimbali kwasababu walitaka kuwa wajuzi katika hayo maeneno. Lakini pia inakuongezea uzito kwenye profession yako, kwasababu inakuwa ni kitu ulichokuwa unakifanyia kazi mwaka mzima.

businesspeople with pens in hands examining schemes on papers

4. Utaifanya peke yako au na watu?

Kama unapenda kuifanya na watu, je akina nani? Unaweza ukafanya na mtu/watu na wakawa wavivu at the end unajikuta unafanya vibaya kwasababu watu uliowachagua kufanya nao walikuwa wabaya. Mwanzoni wakati unaipresent unaweza ukachagua mtu just tu ili upewe hiyo title na uiafanyie kazi, but nashauri uwe makini toka muda unaopresent katika kuchagua watu kwasababu ukiwa makini toka mwanzoni hautokuwa na rush ya kuchagua mtu tu, this is your education, so be smart about it.

5. Usiogope kupata guidance ya walimu toka mwanzo

Kitu nilichokosea mimi ni kutofuata walimu toka hata hatujapresent title, walimu sio maadui zako, most of them wanapenda kukusaidia. Nashauri uende kwa mwalimu akakusaidie kuijenga idea yako vizuri ya project, na kwa vile anajua weakness zako and strength, au kwakuwa utamwambia ataishape idea yako vizuri.

In addition to that, nashauri kila ukimaliza kuandaa report yako unaisave kwenye Drive/Dropbox/ flash ama email. just in case ikitokea ukaibiwa computer au chochote kikaharibika report yako bado utabaki nayo, i had a friend aliibiwa laptop, ila bahati nzuri alikuwa na report yako kwenye hardcopy kwahiyo akaanza kuitype tena mwanzo mwisho. ila ukiwa na backup namna hiyo, haupati tabu.

Na kama umezingatia yote hayo, lakini bado unaogopa kwamba you don’t know what you are doing, usijali. We all didn’t know what we were doing, i started my project na so much fear. Not knowing kitabu chenye page 50 kitatimiaje, nitaandika nini na data nitatoa wapi. Nilichagua topic ninayoipenda ila sikujua what was gonna be the end, lakini at the end of the day nikamaliza project. So usiwaze sana, you will be alright, ask guidance kutoka kwa supervisor wako and ask our very own uncle Google. + Pray alot Mungu akutetee kwa masupervisor.

Eunice

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate ┬╗