Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Jinsi ya kusafiri safari za mikoani comfortably (Kujiandaa na safari ndefu)

Wakati naenda chuo mwaka 2014, ndio ilikuwa mara ya pili kutoka Dar na kusafiri. Mara ya kwanza ilikuwa nilipokuwa darasa la nne, na safari iliandaliwa na mama maana nilikuwa mdogo. Kwakuwa nilisoma chuo mkoani nilisafiri sana na kusafiri kumekuwa sehemu ya maisha yangu kwa sasa.

Na Leo natamani nishare vitu ambavyo navifanya ili kusafiri comfortably lakini pia vile ninavyojiandaa kwa safari..

1. Naandika list ya vitu ninavyotaka kuvibeba ili nisivisahau wakati wa kupaki

Kuna muda tunapata idea ya kupaki kitu ila unasema nitakumbuka. Na kwavile muda wa kupaki najikuta nawaza sana nikaanzisha system ya kuandika kwenye notebook ya kwenye simu mara tu nikumbukapo. Mimi sio wale wanaowahi kupaki, napaki leo, kesho safari. So nikiviandika chini inakuwa rahisi kukumbuka.

2. Kuhakikisha tarehe ya safari na kubook mapema.

Hasa kama unataka kusafiri kwa treni, kubook mapema ni jambo la msingi, lakini hata kwa basi ukibook mapema unapata seat nzuri zaidi.

3. Kupack vitu vya muhimu kwenye mabegi tofauti.

Kama unabeba begi dogo unaweza kuweka vitu vichache vya muhimu na lingine ukaweka vingine na likakaa kwenye boot.

Ila kwenye begi unalokaa nalo unaweza kubeba vitu vfuatavyo vitakavyokusaidia kuwa comfortable kwenye safari:

-Toilet paper
-Neck pillow or any pillow
-Food and water
-Good book/music
-Mtandio or shuka au sweater kama itakuwa baridi njiani

-Pad (just in case, hata kama sio siku zako)

4. Sinywi maji mengi the day before

Well, mi niwale wanaosimamishaga gari ili kuchimba dawa, na ndio maana napendeleaga usafiri wenye choo kama treni. Lakini nikisafiri na basi nahakikisha sinywi maji siku moja au mbili kabla.

5. Kufuatilia hali ya hewa ya ninapokwenda ilinijiandae nguo za kupaki

Well, hayo ndo machache ninayoyafanya yanayonifanya nisafiri comfortably, safari za mbali.

6. Kubeba hela ya change kwaajili ya kuendea nayo msalaani gari likisimama

Hela ya change ni muhimu sana kwasababu inasaidia kutobaki unasubiri change baada ya kujisaidia lakini pia kutoacha kwenda msalani kwasababu hauna hela ya karibu

Also, usisahau kusali kabla haujaanza safari.

Eunice

One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป