Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Maisha ya kila siku,  Random

Jinsi ya kujua kama unatapeliwa mtandaoni (online scams)

Wakati nipo sekondari nilipokea barua pepe.

Kuna mdada ambaye alikuwa na wazazi wake ambao walikuwa ni mabalozi na watu maarufu kwenye nchi yao, ila waliuawa kwasababu ya vita na mambo ya kisiasa.

Binti yao ambaye ndiye aliyebakia mzima kwenye familia hiyo alikimbilia nchi nyingine, na nchi zote zililuwa za Afrika Magharibi sema nimesahau majina ya hizo nchi na sitamani kusema nchi ambazo sizo.

Basi akaniambia hiyo nchi aliyokimbilia yeye anakaa kanisa katoliki kwa padri, na huyo padri nimeongea naye mara kadhaa na mara nyingine alikuwa ananiambia tutaongea baadae maana anaenda ibadani.

Pia alisema baba yake amemwachia mali nyingi sana, ila anatamani apate hela ili aweze kuzitoa hela zile kwenye akaunti aliyoachiwa na baba yake ambayo ipo nchini mwao, kumbuka yeye alikmbia kwa vile wazazi wake waliuawa nchini kwao.

Niliguswa sana na stori yake, na kipindi hicho sikuwa na smartphone basi nilikuwa naenda internet cafe kufungua email ili nichati naye.

Baadae akanipa namba yake, na nikawa naweka vocha nimpigie.

Nampigia nchi nyingine, ambapo nampata padri, akiwa huru naongea na huyo binti.

Akanitumia picha zake nikamjua.

Akanitumia barua pepe zenye upendo huku akiniharakisha nimtumie pesa ili atoe zile pesa alizoachiwa urithi na aliniahidi akizitoa atanipatia nusu, atakuja Tanzania, kuishi nasisi nyumbani kwetu.

Na nikawaza kwa vile ana hela, tutakuwa mbali kimaisha akitupatia nusu ya hela zake.

Basi nikambembeleza mama tumtumie hela, uzuri ni kuwa nilikuwa nafuraha sana ya yeye kuja na kupata rafiki huyu wa ‘nchi za nje’ kiasi kwamba nikawa nawaambia watu.

Mjomba wangu wakati namsimulia ndio akaniambia acha kuchati naye, huyo ni tapeli wa mtandaoni.

Sikumbuki stori vizuri iliishiaje mpaka wakaacha kunitafuta ila hapo ndipo mpaka ninapokumbuka.

Utapeli wa mtandaoni umekua sana.

Unaweza kujiuliza wametoa wapi email yako maana wanakucheki moja kwa moja kwenye email, ila mitandao ya kijamii inawarahisishia.

Kuna aina mbalimbali za utapeli wa mitandaoni. Na utapeli huu haubagui, mtu yoyote anaweza kutapeliwa.

Ila kutokana na niliyoyapitia, kusoma na kuangalia videos zinazohusu wizi wa mtandao, hizi hapa ni njia unazoweza kujua kama unatapeliwa:

– Unakutana na mtu mtandaoni ambaye humjui ila ana stori ya kukugusa

– Mahusiano yenu yanakua kwa uharaka sana

– Mara nyingi stori yake inahusisha pesa, iwe biashara au alikuwa mtoto wa mfalme nk

– Anakulazimisha kutuma pesa baada ya kumjua kwa muda mfupi sana (kumtumia haraka)

– Stori yake au hela yake anayokuambia anayo inaonekana ni kubwa sana kwa hiuo stori kuwa ya kweli. Yani kila ukiifikiria, stori haikuingii kichwani.

– Unaombwa vitu vya siri kama password benki nao

– Hakuna uhakika wa hilo swala zima zaidi ya maneno yao tu

– Unahisi unafanya dili na kampuni ya kweli na kunwa iliyopo nje (lakini pia ukiangalia google website yao, pale juu hauoni kufuli au https:/)

– Mtu usiyemjua anakutafuta au email usiyoijua kabisa. Anakubembeleza urafiki au kukuelezea shida mara nyingi ni kwa kutumia barua pepe


Ukiwa mtandaoni kuwa mwangalifu sana. Usijaze jaze form bila kuzisoma na pia usitoe habari zako za siri kama password ya benki nk.

Je, ushawahi kutapeliwa mtandaoni?

Nisimulie story yako

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป