Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Mambo 9 unayoweza kufanya kusherehekea Krismasi chuoni (Kama hauna test)

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Krismasi chuoni inaweza kuwa siku ya test, siku ya upweke na kukumbuka nyumbani au siku ya kukubaliana na maisha ulionayo na kufanya vitu vitakavyokufurahisha siku hiyo.

Kwanini malecturer wengine hutoa test siku za sikukuu, ni jambo ambalo hatuwezi kulielewa, ila kwa vile upo chuo inabidi tu ufanye kwaajili ya masomo yako.

Kwa wale wasio na test leo, haya hapa ni mambo kadhaa unayoweza kuyafanya kusherehekea siku ya leo;

Nenda katembelee ndugu

Kama upo sehemu ambayo una ndugu au jamaa, na wamekukaribisha au unajikaribisha, leo ndio siku nzuri ya kwenda.

Mbali na ndugu unaweza pia kuispend na wale unaosali nao, mimi nimekula Krismasi kwa mchungaji wa kanisa nililokuwa nasali chuo, kwahiyo inawezekana.

Kaa nawanaroom au amueni kutoka pamoja au kusherehekea pamoja

Kama una mahusiano mazuri na wanaroom mnaweza amua cha kufanya kushrehekea, mnaweza peana zawadi, mnaweza kutoka out mkaenda kuspend mahali au mnaweza kaa tu room na kurelax.

Nenda kale sehemu chakula au kinywaji kile unachokipenda / au kipike kama upo off campus

Kwangu mimi sio Krismasi bila Pilau, linaweza pikwa siku yoyote ila la Krismasi huwa tofauti. Dumisha utamaduni wako unaofanyaga, hata kama halitokuwa kama la nyumbani lakini kufanya kile ulichozoea kufanya au kula kile ulichozoea kula siku hiyo kutakufanya ujisikie umesherehekea.

Sikiliza nyimbo za Krismasi na angalia movies zote za Krismasi

Moja wapo ya njia inayokufanya ujisikie upo kwenye sherehe ni muziki, na nyimbo za Krismasi zipo kibao YouTube,na movie pia, tumia siku ya leo ukisherehekea hivyo.

Chat na wengine

Wanachuo na watu wanyumbani, wapigie kuwajulia hali na kuwatakia heri. Tuma zile meseji za kuforward za Krismasi😂😂, connect na marafiki zako pia waliopo mbali na karibu. Kama unajisikia upweke kaa mbali na mitandao ya kijamii siku ya leo utajisikia vibaya tu na kupoteza siku nzima.

Nenda na wale wanaoenda kula sikukuu na watoto wa vituoni

Kama kuna vikundi vimepanga kutoa muda na fedha kwa vikundi fulani ni vizuri kushiriki, unapotumia muda wako kuspend Krismasi na hao watu au watoto na wewe unapata faraja na furaha.

Vaa nguo ya sherehe au mpya

Ni njia ndogo inayokufanya ujisikie kama umesherehekea, nakumbuka huu ulikuwa utamaduni tulipokuwa watoto lakini unaweza kuufanya sasa hivi pia kujisikia kama umesherehekea na kujizawadia mwenyewe nguo mpya.

Unaweza kujinunulia zawadi

Kama unarafiki mnayeweza badilishana sawa, kama hauna jinunulie zawadi wewe mwenyewe, chochote kile kinachokufurahisha.

Unaweza fanya self reflection

Mwaka umeisha huu, ni jambo gani umejifunza, umekua eneo gani, eneo gani ungependa ujiendeleze nk.

Unaweza tumia maswali haya kufanya self reflection.


Nawatakia wanachuo heri na fanaka katika sikukuu hii ya Krismasi.

Unajambo gani ungependa kulifanya mbali na haya? Niambie kwenye comment👇🏿

Follow @maishayachuo Instagram ili kupata dondoo, ushauri na msaada kila siku kuhusu maisha ya chuoni.

Eunice.

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป