Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Self Care

Jinsi ya kujiandaa na Christmas mapema ili usiwe busy kwenye sikukuu yenyewe

Ni miaka minne sasa tangu niwepo nyumbani kwaajili ya Christmas ila nilipokuwepo Christmas ilikuwa busy sana.

Haikuwa Kama sikukuu ambayo unajua lengo lake, ilikuwa Kama shida/mzigo hasa kwa wanawake.

Mtaani kwetu tuna tabia ya kupeana vyakula sikukuu, kwahiyo Kama sikukuu hii ya wakristo, tunawapelekea waislamu.. na hivyo hivyo kwenye sikukuu ya kiislamu.

Kwahiyo asubuhi yake ni kuamkia kupika, kuhangaika, kuzunguka, mpaka unakuja kuoga, ili usheherekee inakuwa saa kumi na sikukuu yenyewe umeichoka. Hapo ndo unatamani ungekuwa mtoto.

Hivyo kutokana na kupitia hayo, nikajifunza jinsi ya kujiandaa mapema na sikukuu ili nifurahie kwenye sikukuu yenyewe.

Mambo yenyewe niliyojifunza ni:


1. Kujikumbusha lengo la sikukuu

Ingawa tunakunywa na kula, lengo kuu la sikukuu ni kukumbuka kuzaliwa kwa mwokozi wetu.

Tusije tukahangaika Sana hata kukumbuka kwenye tukaacha kukumbuka, tukawa Kama Martha kwenye Biblia tukasahau lililo la muhimu.


2. Kufanya maandalizi usiku wake

Kama Kuna vitu umepanga kupika, na ni vingi, ni vyema vingine ukaviandaa usiku ili usije ukapata shida na maandalizi.

Kama unaweza kupika kabisa au ukaandaa tu kesho utamalizia kuvipika, ni Bora kufanya hivyo.

Kama ni usafi pia unaweza kufanya usiku, ili siku hiyo uwe na muda, wakukumbuka au kufurahia na familia.


3. Kuhakikisha mahitaji muhimu ya siku hiyo unayo hasa yanayopatikana mbali

Kama Kuna vitu unatakiwa kununua na vinapatikana mbali, ni heri ukawa navyo ndani ili usije ukahangaika kwenda safari za mbali tena siku ambayo ingekupasa kukaa nyumbani kufurahia na familia.


4. Usihangaike Sana na kutaka kufanya Kila kitu kiwe kizuri ?%

Kuna muda hasa kwa vile sisi tunakaribishaga watu na kupelekea majirani chakula basi tunatamani Kila kitu kiende Kama tulivyopanga.

Kwahiyo tunaanza kupata mawazo na kusumbuka ili kufurahisha watu, na kusahau lengo lenyewe la sikukuu.

Hata vitu vikiwa vizuri kidogo lakini Kuna amani na upendo hakuna haja ya kuiharibu furaha hiyo kwasababu tu maandazi yaliungua na majirani watatuonaje.. Nahisi Kama hicho ni kitu kidogo sana. Ukilinganisha na furaha ya sikukuu hiyo.

Usijipe msongo wa mawazo na kuwaharibia wengine sikukuu, waache kufurahia kisa maneno yako kwa vile wameunguza pilau bahati mbaya.

Sio Kila kitu huwa kinaenda Kama tulivyopanga..


5. Fanya mipango ya vitu vinavyohitajika mapema na kazi ya Kila mtu siku hiyo

Kusaidiwa ni vizuri, na nashauri mkifanya vitu kwa pamoja nyumba nzima mapema Sana mnamaliza mnaendelea na sherehe.

Ni vizuri Kama Kila mtu atajua yeye anafanya nini, wapi, saa ngapi nk, ili kuwepo na msaada wa kutosha usijisikie unafanya Kila kitu mwenyewe ukapata mawazo au ukakasirika sikukuu nzima kwasababu wenzako wamekaa wanafurahi.


Na hayo ndo mambo ambayo yanaweza kukusaidia usiichoke sikukuu kabla haijaisha.

Heri ya sikukuu ya Christmas

Eunice

Translate ยป