Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

thoughtful black man writing in notebook sitting at table in outdoor cafeteria
Dondoo za Maisha,  Guest Post

Siri 10 za maisha ambazo ni muhimu kuzijua mapema

Maisha hayana formula, ila yana siri nyingi sana.. Bwana Reginald Kaijage kaandika siri hizi 10 na nyingine moja ya nyongeza ambazo ni muhimu kuzijua kwenye maisha.

1.Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana “kikulacho kinguoni kwako!”, Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake!

2.Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako!, Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa


3.Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana?


4. Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.


5. Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matundo ndo unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka!, Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona.


6. Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute Kama kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?


7. Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako yote umepiga magoti!


8. Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako alichagua kuyaficha! Kama unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako utaishia kujilaumu sana kwa kuto kumpa baba yako Upendo aliostahili kutoka kwako.

Bonyeza hapa👉🏿 kusoma hii makala kama umekua bila baba maishani mwako


9. Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli kabisa

10. Hata kama umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike

Na ya nyongeza

11. Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee ni hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto zako watayabusu tu!


Imeandikwa na Reginald Kaijage. Email : rrkaijage59@gmail.com

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป