Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Guest Post,  Maisha ya Chuo

Ushauri wangu kwa wanafunzi wa kidato cha sita

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

——

Mwaka 2010 nilikuwa mtahiniwa wa kidato cha sita kwa mchepuo wa PCM, pale shule ya sekondari Pugu iliyoko Jijini Dar es Salaam hivyo naelewa homa ya mtihani ilivyo kwa wanafunzi wengi pale ratiba ya mtihani inapotoka.

Mimi kama baba, lakini pia kama mtu aliyewahi kupita kwenye darasa hili nimeona umuhimu wa kuandika mambo machache muhimu yanayoweza kukusaidia mwanafunzi wa kidato cha sita wakati huu unapoelekea kwenye mitihani ya mwisho;


– Amini kuwa utafanya vizuri Haijalishi

Kujiamini ni silaha kubwa inayowasaidia watu wengi katika kufanya mambo makubwa duniani na Mambo ambayo yanashangaza ulimwengu.

Wakati kama huu mwanafunzi wa kidato cha sita unapaswa kuwa na maneno ya ujasiri kuliko maneno ya hofu .

Jitabirie matokeo makubwa.

Shule yangu ya O’ level ilikuwa na kauli mbiu ya ‘Aim High’ kauli mbiu iliyohamasisha wanafunzi kuwaza kuwa na matokeo makubwa na kuacha alama shuleni.

Usijiwazie kufeli waza kuwashangaza watu ambao wanaona Kama huwezi.

Ndiyo, inawezekana.

Bado unayo nafasi ya kufanya vizuri.

Wale wanasayansi wanakumbuka kuwa “Last drop can change the color of the solution”

Usikate tamaa au kukatishwa tamaa . Bado unayonafasi ya kufanya vizuri Kama utajiamini.

– Tumia makundi ya majadiliano vizuri

Njia ya vikundi vya majadiliano (group discussion) Ni njia iliyothibitika kuwasaidia watu wengi kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani kwa ujumla wake.

Njia hii ndiyo inayomsaidia mwanafunzi kusoma mambo mengi kwa muda mfupi.

Pamoja na ratiba utakayokuwa nayo ya kujisomea mwenyewe jitahidi sana kusoma na wanafunzi wengine pia.

Nakumbuka wakati tuko kidato cha nne mwaka 2007 yapo masomo ambayo walimu hawakufundisha kabisa lakini kupitia makundi ya majadiliano yalitusaidia Sana na darasa letu la mwaka huo(2007) linatajwa kuwa darasa liliofanya vizuri sana.

Yapo matokeo makubwa ya kusoma kwa vikundi.

– Epuka udanganyifu

Ukweli ni kuwa hapa duniani kila mtu anavuna alichopanda. Huwezi kuwa na shamba ambalo ulipanda mahindi baadae ukaja kuvuna mtama.

Ninachoamini ni kuwa mwanafunzi anayejiamini na aliyejiandaa vizuri hawezi kufeli mtihani.

Mwanafunzi aliyejiandaa vizuri na anayejiamini huwa hasubirii mitihani ivuje ndipo afaulu.

Udanganyifu umekuwa ukifanya watu wengi kufutiwa matokeo na kupoteza malengo waliyokuwa nayo juu ya masomo na maisha kwa ujumla.

Ni vema ukajiandaa vizuri kwa ajili ya mtihani wako usitegemee kabisa habari ya mtihani kuvuja au kuingia na majibu (nondo).

Amini kile ulichosoma kuwa chatosha kukusaidia.

Kila la heri kidato cha sita!


Imeandikwa na Joas Yunus, maarufu kama Jyb. Joas Yunus ni mfikiri haraka, mtatua matatizo ya jamii, mwanasayansi, mshauri wa biashara, mwandishi wa vitabu, kiongozi na mjasiriamali kwa shauku.

Mawasiliano: 0656110906, (joasyunus8@gmail.com)
Instagram: @jyb_joas

Share Your Thoughts With Me

Translate »