Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Soft skills unazopaswa kuwa nazo chuoni

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Haijalishi kama unaenda certificate, diploma au degree. Hizi hapa ni soft skills zitakazokusaidia :

Skill ya 1. COMPUTER SKILLS.

We all know, technology inakua kwa kasi sana. Kiasi kwamba kila nyanja ya maisha yetu hukosi impacts za tarakirishi (computer).

Sasa basi…

Chuoni hutoelekezwa basic computer skills zozote …unless otherwise uwe unasoma I.T and its related fields.

Regarding so…utakuwa unajikuta ukitafuta sana msaada kwa vitu vidogo vidogo tu yaani (though hapa, dada zetu hujikuta wanaangukia mikono hatarishi kwao)…ambavyo ungeweza kuvifanya wewe mwenyewe, tena kwa ufasaha wa hali ya juu.

Coming back to the point…

Ukiwa kama mwanachuo mtarajiwa, jitahidi sana kujifunza hivi vitu;
MS Word
MS Excel
MS PowerPoint
Computer Basics

Anza wakati huu kujifunza kdg kdg…hatimae hivyo vitu utavimudu by more than 90%.

Makala inayoendana : Application 9 za smartphone zitakazokusaidia chuoni kama hauna laptop/computer

Hayo mambo yana umuhimu sana kwa maisha yako ya chuo… Ufanyaji wa Assignments (Individually or Group), na Uwasilishaji wa Modules …hutegemea sana hizo MS Office.
Sasa usipokuwa na knowledge hata kdg kuweza kutumia vyema hizo MS Office… kuwa tayari tu uwe exploited na wahuni wa chuo.

Kuna kitu ambacho pia mnapaswa kujua…

University graduate ambaye hana hizo Computer Skills huumia sana kwenye suala la ajira…(tusiongee sana huku, ila mkifika mtaelewa).

2. COMMUNICATION SKILLS.

Hapa ujijenge namna ya kuwasiliana vizuri na watu wanaokuzunguka chuoni na viunga vyake.

Kuwa mtu mwenye kuzungunza kwa heshima na unyenyekevu wakati wote.

Vyuoni kuna kila aina ya watu…tena unaenda kukutana nao ukubwani na wala hujui historia yao.

Hivyo basi…kuwa mtu wa kujishusha na sio kujikweza, kuringa wala kuonyesha nyodo. Hii itakusaidia kuwa mtu pendwa na watu wanaokuzunguka.

Jifunze kupangilia maneno yako vizuri, kuzungumza lugha fasaha (maneno ya kihuni yaache)…kama ni kwa kuandika, andika kisomi…zile ‘xx’, ‘pw’, ‘ky’ …zipunguze, ushakuwa mtu mzima sasa.

Kwa upande mwengine wa shilingi…

Ni vyema kuanza kujijenga kwenye kuzungumza, kusikiliza na kuandika lugha ya kingereza.

Lugha ya kingereza hutumika 80% to 90% vyuoni…kuanzia matangazo ya vyuo, class notes mpaka uwasilishaji wa assignments (Presentation).

Makala inayoendana : Njia 6 za kujifunza kingereza bure na kwa haraka

Sina maana kuwa lugha ya kingereza ndio kipimo cha akili, la hasha! Bali tunajikuta hatuna jinsi kwa sababu ndio Instructing/Teaching/Lecturing/Tutoring Language…isipokuwa tu kozi ya BA. in/with Kiswahili…ila ona sasa, hata kozi yenyewe imepewa jina la kingereza! 😂

3. GOOGLE SKILLS.

Chuoni bila internet ni kama gari lisilokuwa na mafuta.

Unajua kwa nini!?!

Mafunzo ya vyuoni yanafuata International standards…though uwasilishaji ama namna ya ufundishaji huwa tofauti tofauti…lakini wote mnatazamia sehemu kuu moja.

Sasa basi…utajikuta unahitaji sana Internet ili kuperuzi sehemu mbalimbali na kuongeza ujuzi wako juu ya jambo flani ktk masomo yako.

Na ndo hapo sasa, Google Skills zinahitajika.

Anza sasa, kujizoesha namna ya kutafuta taarifa yoyote ile kwa kutumia Google Search Engine (Google.com).

Hii ni sawa na kwenda kuvua samaki. Ukienda kichwa kichwa utajikuta unakosa unachokitaka, unakasirika na mwishowe kurudisha mtumbwi nchi kavu. Ilhali kuna mwenzio akienda anarudi na samaki wa kutosha. Utasema ni uchawi, hapana. Ni ujuzi tu.

The same kwenye kutumia Google kusaka maarifa. Take your time kujifua namna ya kutafuta data Google…mpk ufike chuoni, mambo yatakuwa slope tu.

Kwakuongezea…

Kuna jamaa yetu hapa anaitwa YOUTUBE.

I assure you, hakuna Tutorial utaikosa YouTube…hakuna aisee. Hata video ya kufundisha kuchemsha maji ipo. Katafute “How to boil water” utaona.

Too bad, bahati mbaya sana…wengi wenu mnaenda kuangalia nyimbo tu na maumbea…sawa ni maisha yenu, ila mnapoteza madini.

Anyways…

Just use well this time…kuingia YouTube na kujifunza mambo kadha wa kadha…kajipe mwanga kidogo kidogo juu ya scope utakayoenda kusomea chuoni.

Mpaka uje kufika chuo…hutopata tabu sana kuelewa modules…kwa maana utakuwa na ujuzi wa kuipekua pekua YouTube ukapata madini unayoyataka and at the same time utakuwa na ABCs za field yako.

MENGINEYO

Anza kujenga mazoea ya kujua healthy tips zote kuhusu mwili wako. Yes, mwili wako. Kwa sababu kila mtu ana strengths na weaknesses zake za kiafya.

– Eat well & healthy. Usile tu kisa una njaa. Kula kwa afya. Kula mlo kamili. Mwili wako haujengwi kwa matofali.

Boresha muonekano wako, wa nje na wa ndani. Yes, your physical appearance. Fanya mazoezi madogo madogo kujiweka fit. Usikae kizembe zembe. Do Home Workouts. Thank me later.

– Personal Hygiene. Sidhani kama kuna ambaye hakusoma Biology alivyokuwa kidato cha pili. Go and review your notes about it. Anyways, do whatever it takes to maintain your personal hygiene.

– Tambua tu…afya yako ni asset muhimu sana masomoni…huo mwili wako usiutese kwa kuukosesha virutubisho/madini …utakuja kukushangaza vibaya mno mbele ya safari.


Imeandikwa na Muta (0683676795)

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป