Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Things I wish every first year student should know (Part 2) | Your Guide to University Life

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Katika utangulizi wa mfululizo wa makala hii, Nilitangulia kwa kusema,
‘Katika kila hatua mpya ya maisha kuna mambo usiyoyajua kwa sehemu, ambayo ukiyajua na kuzingatia kwa asilimia kubwa yatakuwezesha kuwa na matokeo bora ya maisha tofauti na asiyeyajua kabisa’.

Makala iliyopita nilitanguliza mambo manne (4) ninayotamani kila mwanachuo mpya ayafahamu. Na Leo tunaendelea tulipoishia… tukianza na jambo la 5.

______________________________

5. BEING A STUDENT IS AN IMPORTANT TIME TO LEARN.

(Ukiwa mwanafunzi ni wakati muhimu sana wa kujifunza)

Katika point zilizopita niligusia juu ya kutumia kila fursa sahihi kwako uwapo chuoni. Nikataja mfano fursa ya kujifunza.

Uwapo mwanafunzi katika ngazi yoyote ile, kisaikolojia akili yako inakaa mkao wa kujifunza, mtazamo wako unakuwa wa kujifunza, kwasababu unajua wewe bado ni mwanafunzi.
Pia Mazingira uliyonayo chuoni yanasupport kujifunza (yapo conducive & supportive for learning). Mfano Uwepo wa Maktaba, uwepo wa wanafunzi wenzako na wakufunzi kwa ukaribu , uwepo wa programs mbalimbali za kujifunza, uwepo wa madarasa yanayokupa utulivu kujifunza, mifumo ya field and practical activities za kujifunza, nk.

Vile vile katika kipindi hiki, hata jamii inakutazama kama mwanafunzi, kiasi kwamba hata ukikosea kidogo unavumilika kwasababu unachukuliwa bado unajifinza.Yaani bado Upo katika mchakato wa kuwa mtaalamu.

-Hivyo kwasababu ni kipindi sahihi zaidi kwa kujifunza, ni muhimu ukakitumia uwezavyo kujifunza yale unayotaka kuyaweza na kuwa Bora.
Maana punde tu utakapomaliza chuo, mifumo iliyopo na jamii kwa ujumla (maisha) yatakudai utaalamu wako. Hakuna atakayekutazama kama mwanafunzi tena. Jamii inatarajia kupata mchango wa ulichojifunza katika miaka yote hiyo chuoni.

Hivyo hakikisha uwapo chuoni unajifunza kwa bidii siyo tu mambo ya Kitaaluma darasani bali hata Ujuzi mpya (new skills) tofauti na profession yako. Hii itakufanya kuwa Bora zaidi na mwenye wigo mpana kiutendaji.

6. IT’S GOOD TO INITIATE AND IMPLEMENT WHATEVER LIFE DREAMS AND GOALS YOU HAVE FROM WHEN YOU ARE A STUDENT.

(Ni vyema kuanza utekelezaji wa ndoto zako na malengo yako tangu ungali mwanafunzi chuoni)

Vyuoni tunaenda kusoma (hili ni lengo kuu). Lakini wengi tunazo ndoto nyingi na malengo ya kimaisha ambayo tunatamani siku moja tuanze kuyatekeleza ili kuyafikia.
Ni watu wengi sana wana mipango mingi juu ya maisha yao baada ya chuo, ambayo akilini wanawaza kuwa ONE DAY YES, au NIKIMALIZA CHUO nitaanza hiki na hiki.
Hilo ni jambo jema, lakini kama lengo lako linaweza kutekelezwa tangu ukiwa chuoni, hakuna haja ya kusubiri mpaka kuhitimu ndipo uanze. Hakikisha unalitekeleza kwanzia mapema kipindi hiki.

Mfano,
Kuna watu wana ndoto za kufikia malengo flani katika vipaji vyao au UJUZI wao. (Either Uongozi, Sanaa, Michezo, Ujasiriamali, au UJUZI wowote ).
Vyuoni kuna platform nyingi sana za kufanyia kazi UJUZI wako. Kwakuzingatia mazingira na fursa za chuo chako hakikisha unatumia kila upenyo sahihi wa kutekeleza ndoto zako.

Mfano
(Gombea nafasi za uongozi ili kunoa uwezo wako, Jihusishe kwenye vikundi vya uimbaji kama wewe ni muimbaji, Anzisha taasisi yako kama una malengo hayo kwa wakati huu, Anzisha hiyo biashara kwa level unayoweza kwasasa, Shiriki maonyesho na Mashindano ya vipaji kama wewe ni wa sanaa fulani, nk)

Umuhimu wa kuanza mapema uwapo chuoni ni kwamba. Itakupa wakati mzuri wa kujifunza, kukua, kutengeneza soko, na kujijenga zaidi, kwa kutumia fursa zilizopo chuoni. Hata ukimaliza chuo kuna hatua unakuwa umeipiga na unakuwa na mwanga kiasi fulani kwajili ya kutekeleza maono yako uwapo mtaani (baada ya kuhitimu) tofauti kabisa na mtu anayesubiri amalize chuo ndipo aanze moja..

7. A GOOD REPUTATION IS SOMETHING WORTHY TO BE GAINED, MAINTAINED AND PROTECTED AS MUCH AS YOU CAN WHILE IN CAMPUS.

(Jitengenezee sifa njema, Ilinde na kuitunza kwa bidii uwezavyo Uwapo chuoni)

Unataka picha gani itokee kwa haraka kwenye akili za watu punde Jina lako linapotajwa.?
Mfano ukisikia jina ADAM MACHALILA (Ni definition gani imekuja akilini mwako juu yangu)
Hiyo taswira iliyokuja imetokana either na uliyoyasikia kuhusu mimi, uliyoyaona kwenye maisha yangu, au unayodhani kutokana na ninayoyafanya, nk.

Kiufupi ni ule mrejesho unaonihusu utokanao na taswira iliyopo juu yangu akilini mwako.

Lakini REPUTATION ni kitu ambacho kila mwanadamu anayo nafasi ya kujitengenezea kwa wengine.
Kupitia Mfumo wa maisha tulionao, mambo tunayoyafanya, Tabia tunazoziishi mbele za watu ,nk. Hivi vinaamua ni namna gani watu wanatutafsiri.

Cha muhimu kuzingatia ni kuwa, unaweza kujijengea mwenyewe REPUTATION Nzuri au Mbaya.

Ni muhimu kujijengea reputation nzuri mbele ya jamii yako. Kwasababu habari zako haziishii chuoni tu , au darasani kwako tuu.
Kuna mahala ambapo jina lako linaweza kukutangulia kabla yako.
Kuna fursa utazipata au kuzikosa kwasababu tu ya jina jema au baya ulilojijengea.

Reputation nzuri inakupa Kibali kwenye jamii. Na mbaya itakuharibia/kuzuia Kibali kwenye jamii.
Je ungependa jina lako likitajwa ije picha gani kwenye akili za watu??
Reputation yako iwe MVIVU au MWENYEBIDII. MUAMINIFU au MBABAISHAJI. MWENYE NIDHAMU au MUHUNI. MWENYE KIASI au MWENYE TAMAA.??
Jina lolote katika hayo unalitengeneza mwenyewe kwa namna unavyoishi mbele za watu wanaokuzunguka.

Everything you do matters and people observes. It creates your reputation which will last for a long time even after CAMPUS life.

-Be conscious and wise in every decision and action you make.
-Consider integrity, honesty and righteousness in all things you do In order to be of a good reputation..

Itaendelea………

______________________________

Usiache kufuatilia mfululizo wa post zetu kuhusu maisha ya chuo.

Au kwenye magroup yetu WhatsApp ya CAMPUS STUFFS.

Follow us on
Instagram;- @ Prepare for University

– Adam Machalila

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate »