Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Things I wish every first year student should know (part 3) | Your Guide to University Life

(Kusoma part 1& 2, bonyeza hapa.)

(Your Guide to University Life ni category yenye makala zinazohusu maisha ya chuo, kuona makala nyingine bonyeza hapa.)

Leo tunaendelea na jambo la 9

9 . TIME IS MORE THAN ENOUGH IN CAMPUS

Hili ngoja niliongelee kwa ukweli ambao ni mchungu hata kwangu binafsi.
Maana yapo mengi pia ambayo sikufanya kwa wakati na mengine yalinigharimu sana Kiasi cha kuhatarisha masomo yangu nilipokuwa chuoni. Na yapo niliyoyafanya kwa wakati yakanipa matokeo mazuri kwenye maisha.

Lakini kadri ninavyozidi kujifunza ndipo naelewa kuwa MUDA UNATOSHA.

Kule sekondari wengi tulikuwa tunatumia kengele. Ratiba ilipangwa na shule kwa asilimia kubwa, na walimu walijitahidi kuhakikisha zinafwatwa, kiasi cha kuwaadhibu wasiofwata ratiba. Uhuru binafsi ulikuwa na ukomo mkubwa.
Lakini Huku vyuoni, hakuna kengele. Ratiba ipo lakini inakupa uhuru mkubwa wewe mwanafunzi kujiongeza juu ya matumizi ya muda wako. Hivyo matumizi ya muda yanabaki chini ya maamuzi yako kwa asilimia nyingi zaidi.

Yapo mengi ya kujifunza kuhusu muda. Nashauri baada ya Ujumbe huu Tafuta kujifunza zaidi. Mimi NITAKUPA tips (dondoo) chache tu, zitakazokusaidia kuutumia muda wako vizuri.

a) Amini kuwa muda ulionao unakutosha.

-Mara nyingi sana tunajikwamisha wenyewe kwa kuweka visingizio kuwa tuna mambo mengi, muda hautoshi, tumebanwa, tumetingwa na majukumu,Nk. Kiasi kwamba hakuna hata jambo moja tunalolifanya kwa ubora kiasi cha kushuhudia kwa ujasiri matokeo ya huko tunapopeleka muda mwingi.
Matokeo yake tunakuwa watu wa ubize mwingi uliojaa excuses nyingi lakini matokeo hayaonekani. Ni kwasababu ya mitazamo na tabia.

Iko hivi;

-Miongoni mwa vitu ambavyo wanadamu hatuwezi kujitengenezea ni pamoja na muda. Tuliukuta duniani na tutauacha. Muda ni rasilimali inayojitegemea, hatuwezi kuuzidisha, kuupunguza wala kugawana muda. Kwamba mwenye mwingi ampe mwingine. Kila mtu anaoperate ndani ya masaa 24 kwa siku.

– Hivyo _wajibu wetu ni kujiongoza na kupanga namna ya kuutumia huu muda ili tupate matokeo tunayoyataka._
-Ukiwa na mtazamo huu, itakusaidia kama msingi wa matumizi yako ya muda.

b) Zingatia Vipaumbele
(prioritization)
-Do the first things first.
-Mfano. Kwasababu ni wanafunzi then, Ratiba zako zoote zinatakiwa kutoa kipaumbele Kwa Ratiba za Masomo Chuoni kwasababu ndo kilichokupeleka.
-Chuoni kuna ratiba za Jumla zinazoongoza shughuli zote za Chuo ambazo jamii nzima ya chuo inatakiwa kushikamana nayo Accordingly.
Mfano; Ratiba za vipindi vya masomo, mitihani, matukio maalumu ya chuo (graduations, uchaguzi, G.As, Symposium,nk. Kulingana na utaratibu wa chuo). Mara nyingi hutolewa mapema ili jamii nzima katika chuo izingatie ratiba hizo pale inapopanga ratiba nyingine ndogo ndogo. Tafuta PROSPECTUS na Almanac ya chuo, course outlines kwa kila somo zitakupa Dira hapo chuoni.

-Hivyo hakikisha ratiba zako binafsi haziingilii ratiba za chuo zinazokuhusu.
Mfano, Jitahidi Usipange majukumu binafsi ndani ya muda wa mitihani , Vipindi, nk.
Isipokuwa tu, pale inapotokea dharura ya lazima isiyoweza kuzuilika. Ambapo hakikisha unafwata utaratibu rasmi za chuo ikiwemo za utoaji wa taarifa ili uwe salama (safe side).
Japo kiuhalisia ni watu wengi hupanga ratiba zao kinyume, ila ni risky.

-Hii itakusaidia kuwa focused na kukuongezea ufanisi kiutendaji kwa kukuepusha na frustration . Pale ambapo unafanya shughuli fulani ila huku una wasiwasi na kinachoendelea darasani, utajikuta umakini unapungua na ufanisi unashuka.

c). Fanya kazi ndani ya wakati
-Epuka kusubiri deadlines zikaribie ndo uanze kufanya assignments au kazi yoyote. Kazi yoyote ukiianza mapema utakuwa na muda wa kutosha kuirekebisha, kuifanya kwa umakini mkubwa na inakupa guarantee ya kuifanya vizuri kwa asilimia kubwa.

d). Fika mapema.
-Kwenye vipindi, Vikao, mitihani, nk. Azimia kufika mapema. Itakupa utulivu mzuri utakaochangia ufanisi na kujiandaa vizuri katika kile unachoenda kufanya.

e) Manage distractions. (Thibiti vitu vinavyoingilia majukumu yako ya wakati husika)

-Uwapo katika majukumu yoyote kuna vitu vinavyoweza kuingilia muda wako katika majukumu fulani. Mfano , kupiga story , matumizi ya simu yasiyo ya lazima / kwa muda mrefu, safari zisizo za lazima,nk.
-Hakikisha unakuwa na kiasi, jitahidi kuthibiti kila kitu kinachoweza kuiba attention yako ndani ya muda wa jukumu fulani.
-Amua kufanya unachopaswa mpaka kikamilike ndipo ufanye mengine ya ziada.

f). Fanya maandalizi ya awali ya matumizi ya muda.
-Andaa to-do List kabla ya muda.
– Orodha ya mambo yote unayotaka kuyafanya kesho, iandae Leo. Ya wiki ijayo iandae kabla ya wiki kuanza.
-Weka list yako kwa kuzingatia vipaumbele, anza na jukumu la muhimu zaidi. Kisha yawekee muda majukumu yote (kila jukumu ujue utalifanya kwa muda gani na saa ngapi )

g) Heshimu muda wa wengine

-Kama ambavyo utaheshimu muda wako vilevile usiwe distraction kwenye muda wa watu wengine.
-Heshimu muda wa wanafunzi wenzako mnapokubaliana kufanya jambo fulani kwa pamoja, usiwe kikwazo kwa kuchelewa au kufanya kinyume na makubaliano.
-Muda wa wakufunzi pia ni wa kuheshimiwa. Ukielekezwa kuwa mwalimu atahitaji kazi fulani kwa wakati fulani au atakuja kwenye kipindi muda fulani, hakikisha unazingatia na kutekeleza.

________________________
Matumizi makini ya muda yanatuwezesha kufanya mambo yanayoonekana ni mengi sana ndani ya wakati huohuo ambao wengine wanaona hautoshi.

Haihitaji kusubiri ili uanze. Anza sasa hivi, chukua karatasi uanze kuandika to-do List yako ya muda uliobaki leo na kuendelea..

REMEMBER; Any time you save, is time for you

Tukutane tena wakati mwingine kwajili ya mwendelezo.

Adam Machalila

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate »