Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo,  Self Care

Kwa anayeona chuo kigumu, hauko peke yako, hizi hapa tips za namna ya kusurvive

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Ukweli ni kuwa tofauti na tunavyoambiwa Mara nyingi, chuoni sio bata.

Maisha ya chuo ni magumu, kwa mwaka wa kwanza na muda mwingine hata kwa miaka inayoendelea.

Nakumbuka kama nilikuwa na test mbili za miaka tofauti ambazo nilipata zero.. Kwahiyo naelewa.. Kuna muda nilikuwa nahisi mwalimu anachofundisha sitokuja kukielewa.

Au hata ameitoa dunia gani mbona hakieleweki?

Kuna muda niliwaza nafanya nini chuoni? Au sina akili? Hivi kweli nafaa kuwepo chuo au niache tu?

Ila nikiacha nitafanya kitu gani?

Nilikuwa confused na sikujua cha kufanya honestly kila siku najivuta kwenda darasani ambapo sielewi kitu, narudi room nimechanganyikiwa zaidi ya nilivyoenda darasani.

Kwa ambaye unaona chuo kigumu, naelewa unachomaanisha. Hauko peke yako. Na Mimi pia nimepitia hilo.

Nahisi mwaka wa kwanza unakuwa mgumu kwasababu vidato vya chini, ni kama vinafanana. Mfano high school ni mpya lakini ni muendelezo wa physics ambayo umekuwa unaisoma toka sekondari, lakini chuo mambo yanakuwa mapya kabisa.

Kwahiyo ule upya, ule uhamisho wa kuacha kabisa high school na kuingia mazingira mapya kabisa ya chuo, ule ndio unaotisha. Ule ndio mgumu.

Mazingira mapya, masomo mapya, walimu wapya, maisha mapya.

Hizi hapa tips ambazo zilinisaidia Mimi, I hope zitakusaidia na wewe pia:

– Kusoma kwa discussion

Hasa kama hauelewi darasani, tafuta mtu unayemuona ameelewa, soma naye. Mimi nilipata bahati ya kusoma na best student wetu, kwa miaka yote niliyokuwa chuo. Kwavile nilijijua sipati kitu discussion ya wengi, nilitaka kuwa na discussion na mtu mmoja. Alikuwa ananielekeza ila pia nilikuwa namuuliza maswali niliyokuwa naona magumu. Thanks Paul?.

Usidodge darasani

Kitu nilichokosea ni kutokwenda darasani. Hasa katika masomo magumu na niliyoona sielewi, hii haisaidii. Honestly inakuletea hata uadui na walimu wa masomo hayo kitu abacho haukitaki Hasa kama somo lake tayari haulielewi.

Kuongea na watu wa nyumbani

Muda mwingine unakuwa umekumbuka nyumbani au unaona unapata shida bora urudi nyumbani. Kuongea na nyumbani na kuwaambia vile unahisikia huwa inasaidia. Kuongea nao kunakufanya ujisikie uko nao karibu, hii inapunguza kuwakumbuka.

Kutengeneza urafiki na watu

Ni mazingira mapya na kama hakuna watu uliosoma nao huko nyuma basi unanza upya kutengeneza urafiki na watu. Ila kuwa na social life kunasaidia, kuangalia tu movie peke yako kitandani kwako hakusaidii, kunazidi kukufanya uwe chini, ila kusocialize na watu kuna kufanya uone shida imepungua, lakini pia hautojihisi uko peke yako.

+ Unaweza kujiunga na vikundi ambavyo wanafanya unachokipenda either michezo, gym,chapel nk.. Hii ni njia rahisi ya kupata marafiki, na kwa vile wanafanya unachokifanya inakuwa rahisi kuzoeana.

Lakini pia jitahidi kuyajua mazingira uliyopo, ijue campus yako pia.

be kind to yourself / don’t beat yourself up

Ni mazingira mapya, mabadiliko mapya kabisa. Mi naamini kila mtu ana akili, mpaka umefika hapo basis una akili.. Kwasababu tu hauelewi hilo somo haimaanishi wewe ndio mjinga sana kwenye maisha, au wewe ndo the biggest loser. Hapana, ni mabadiliko, utachukua muda kuyazoea, be kind to yourself, you are doing the best you can. Una akili, don’t beat yourself up. Jitie moyo.

Taratibu things will get easier

Mfano kubalance muda, kupata madarasa/ lecture halls kiurahisi, na hata kwenda mjini bila kupotea.. Taratibu utazoea, utapata marafiki nk. Niamini, things will get easier, na kama ndivyo maisha yako yanavyotakiwa kuwa utagraduate.. Utamaliza na kuendelea na mengine. Things will get easier, mwanzo tu ni mgumu.

Omba msaada

Chuo chetu tulikuwa na mshauri wa wanafunzi lakini pia hata dean of students anaweza kuwa msaada. Tafadhali kama unataka msaada au mtu wa kuongea naye, omba msaada usijisike aibu au kuogopa. Omba msaada/ushauri kwa watu Hawa, tafuta mtu wa kuongea naye umwambie unavyojisikia au hali unayopitia, hauko peke yako.

Follow Instagram akaunti hii kwaajili ya wanachuo ambapo kuna tips zitakazokusaidia kukabiliana na changamoto za chuo.

Pia watumie marafiki zako hii makala pia, hauwezi jua wanajisikiaje kuhusu maisha ya chuo, watie moyo.

Eunice

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »