Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Ujumbe wangu kwa vijana wote waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Kwa kuzingatia hali ya taifa letu, hali za maisha ya familia nyingi za kitanzania, nimetamani sana kuongea na wewe kijana uliyepata neema ya kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu.

Natamani kwanza ufahamu yafuatayo.

1. Umefika hapo kwa Neema Tu.

Najua unafahamu ni kwa namna gani wengi walitamani kupata hiyo nafasi, wengi walifaulu zaidi yako, wengi walikua na uwezo mkubwa wa kifedha zaidi yako lakini hawajafanikiwa kupata hii nafasi, Mshukuru Mungu kwamba amekuwezesha. Don’t take it for granted

2. Kwa hatua ulioyofikia , Fahamu kwamba Taifa, jamii na familia zina matarajio makubwa sana na wewe, kuna mabadiliko tunatarajia kuyaona baada ya wewe kufika chuo kikuu.

3. Mpaka wewe kufika hapo kuna watu imewagharimu pesa zao, nguvu zao na vitu vingi sana mpaka wewe kufika hapo ulipofika.Usichukulie poa!!

Kwanini nimetamani kuongea na wewe ?

Kwasababu nimeona kuna hatari kubwa sana ya wewe kupotea kama hautayajua haya mapema. Niliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu miaka kadhaa iliyopita hivyo kwa kuona, kushuhudia na kujifunza kutoka kwa wengine nimeona nina kila sababu ya kukushirikisha ili USIJE UKASEMA HUKUJUA.

ELEWA….

1. Chuo sio mahali pa “Show off” ni mahali pa kuongeza ulewa wako, kutanua wigo wa watu “Connection” kujifunza mambo ya msingi ya kukufaa kwenye maisha yako. ukienda chuo na mentality hii ya “show off” utaishia pabaya. Maana itakulazimu kuishi maisha “Fake” ambayo YATAKUGHARIMU.

2. Chuo sio mahali pa kuanza kufanya UJINGA wala KUJIACHIA ila ni mahali ambapo UFAHAMU & AKILI YAKO inatakiwa kukua. Sio mahali pa kwenda kuanza ku practice vitu vya kijinga kama na vitakavyokusababishia madhara makubwa sana hapo baadae mambo kama kunywa pombe, kwenda clubs, kuvuta bangi hayana faida yeyote. Tunatarajia kuona akili yako imekomaa na hufanyi ulimbukeni wa aina yeyote.

3. Chuo sio mahali pa kwenda kuanzisha ndoa zisizo rasmi. Binti unayeenda Chuo kikuu, kule huwa “kuna ndoa za msimu” watu huoana kwa semester na kuachana. Ni vyema ukatulia na ku focus kwenye mambo ya msingi sana, sidhani kama wazazi wako wanakupeleka chuo kikuu ili ukawe mke wa kupakua na kupika au ukawe mume wa mtu. Usije ukakubali kuishi na kijana kwa sababu yeyote ile isiyo ya msingi. Jambo hili limeleta madhara makubwa sana ya kimasomo, kiafya na hata ki akili (Ki_saikolojia) Hasa kwa wadada wengi sana. Sitamani ukawe ni moja kati ya watu watakao sema “Ninge”. Wengine wameshika mimba zisizo tajariwa kwasababu ya kukosa ufahamu wa kutambua nini kifanyike wapi na lini. Utafiti unaonesha asilimia 90 ya ndoa za msimu za chuo huwa zinavunjika baada ya masomo kuisha.

Achana na “Vi desa boy” (Desa boy ni wale wakaka wanaojitolea kukusaidia kwenye masomo na malipo yao huwa ni mwili wako) chanzo cha hawa desa boy ni UVIVU na KUTOTAKA KUJITUMA na KUPENDA MITEREMKO kwa wasichana wengi.

4. MARAFIKI, ukifika chuo kikuu unakutana na watu wengi kutoka sehemu tofautitofauti. Kuwa makini sana unapochagua nani awe rafiki yako, kwasababu hawa wana nafasi kubwa sana ya kuharibu maisha yako au kujenga maisha yako. Unapochagua marafiki, kumbuka ulikotoka, kumbuka familia yako Wapo walioenda kupoteza muda kwasababu wana urithi tayari, wewe mwenzangu na mimi ambaye huna urithi hata wa baskeli mkweche usije kujichanganya. “Ndugu huwezi kuchagua ila marafiki unaweza kuchagua”

5. Chuo sio mahali pa MASHINDANO. Usiende chuo kushindana na mtu yeyote kwasababu hujui alikotoka. Ishi maisha yako. Chuo watu huwa wanashindana kuvaa, kubadilisha nywele nk. Nenda karidhike na maisha yako, sio lazima uishi maisha yasio yako, kama uwezo wako ni kuvaa nguo za elf 5, Boutique waachie wenye uwezo nazo, kama uwezo wako ni kusuka Yebo fasta. Brazilian hair waachie wanaojiweza. Kaka kama uwezo wako ni kuvaa kadeti ya elf 10, mambo ya fashoooooon waachie wanaojiweza. Na kama ukibahatika kupata “Boom” Litumie vizuri.

6. Chuo sio mahali pa “Kuharibu maadili” ni sehemu tunayotarajia kuwe na maadili mazuri kuliko mahali pengine popote kwasababu tunafahamu mahali hapo wamejaa watu wenye uelewa na wanafahamu nini maana ya maadili. Hatutarajii kukuta msichana wa chuo kikuu unatembea uchi kwasababu tunajua sasa upo matured enough kutambua nini cha kuacha wazi na nini cha kuficha. Tunawapa tabu sana wanajamii kuelewa nini maana ya chuo kikuu, wengi ukisema yupo chuo kikuu wanapata picha ya “Atakua anavaa nusu utupu, starehe, nk” Ni sisi ndio tumeharibu hii image. Nenda kawe na Maadili yanayoendana na Tamaduni za kitanzania.

7. Chuo ni mahali pazuri sana kwa kumtumikia Mungu. ANGALIZO, Hapa lazima U balance, kuna watu wengi sana walifika chuo baada ya kujiunga na vikundi mbalimbali wakaacha kabisa kilichowapeleka chuo na hatimaye wakashindwa kuendelea na masomo. Mimi ni shahidi, Hakuna mafanikio bila Mungu lakini be aware!! Mungu ni wa utaratibu, wakati wa vipindi nenda kwenye vipindi, wakati wa discusion nenda discusion na wakati wa fellowship nenda fellowship.

8. Chuo ni mahali pazuri sana pa kutengeneza maisha yako, kutengeneza connection, kutumia vipaji ulivyopewa na Mungu, ni platform nzuri ya kutengeneza kesho yako. Ukifika chuo usizubae, Fanya bidii Darasani lakini hakikisha “Unacheza miguu yote miwili kama kaka Sam Sasali ambavyo huwa anasema akimaanisha soma lakini vilevile noa kipaji chako, tumia uwezo wako vizuri.

Soma vitabu vya Darasani lakini tafuta na vitabu vya maisha ambayo ni tofauti na vya Darasani.

SASA BASI; Kuna maisha baada ya chuo na haya yanatengenezwa the moment unaingia chuoni. Kumekua na janga kubwa la wasomi wenye frustrations na stress; pamoja na sababu zingine lakini mojawapo ni KUTOKUJIANDAA WAKATI YUPO CHUO wengi wanaanza ku save hela mwaka wa mwisho, wengine wanashtuka semester ya mwisho na wengine wakifika mwaka wa tatu ndo wanapanic.

Ukiwa chuo Jiandae, kama unapenda biashara anza kufanya taratibu taratibu. JIANDAE MAPEMA. Kumbuka; Elimu haipimwi kwa Idadi ya vyeti ulivyonavyo bali kwa MATOKEO CHANYA UNAYOLETA KWA FAMILIA YAKO, JAMII YAKO NA TAIFA KWA UJUMLA.

AMINA SANGA
0654999828

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate »