Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Career Guide

Ujuzi tunaoudharau lakini una pesa nzuri mtaani

Nakumbuka kuna siku nilikuwa Dodoma na nikawa nashona viatu, fundi viatu akawa analalamika jinsi jamaa aliye ofisi ya juu ghorofani humdharau kwa kumuomba apunguze hela na kumlalamikia kuwa anahela za juu wakati akienda kununua vitu supermarket haombi bei ipunguzwe, akasema ‘kama anaweza kufanya yeye si afanye’

Baada ya muda akapita muendesha mkokoteni na fundi akaendelea kusema, ‘yani tunadharauliana tu ila kila kazi ya mmoja wetu inatupa chakula, inaendesha maisha yetu lakini pia ina umuhimu kwenye maendeleo yetu binafsi, ya jamii na ya nchi’

Pia Soma : Kudharauliana kutaisha lini?

Ukweli ni kuwa wengi wetu, hasa tuliopitia chuo kuna kazi tunazidharau. Lakini nisiwe kauzu sana kwa walioenda chuo, hata kawaida tu mtaani kuna kazi watu wanadharaulika kwa kufanya, kuna kazi zinaonekana za wasiosoma au za watu ambao hawastahili heshima, wa daraja la chini. Badala ya kuonekana kama sehemu ya kujipatia kipato inaonekana ni sehemu ya kupima hadhi na heshima ya kumpa mtu kutokana na kazi yake. Hapo ndipo tumejikuta wengine tunadharau na kuacha kutafuta kipato kwa kazi fulani kwavile tunaogopa dharau au kuonekanaje mbele za watu.

Lakini tunasahau kuwa kuna watu wanafanya kazi hizi na wanaendesha maisha yao, kuna watu wanafanya kazi hizi na wanajiendeleza nk sasa basi kama umemaliza chuo au bado uko chuo unaweza kutafuta ujuzi huu na ukawa na ujuzi mwingine unapokuja mtaani ili uwe na pakuanzia hata ukiwa hauna ajira.

Na kazi hizo ni;

– Kutengeneza juice, ice cream nk

– Kupika bites

– Kuuza duka

– Dereva bodaboda

– Udalali

– Kutengeneza matofali

– Kilimo

– Mpaka rangi, mjenzi na muweka tiles

– Fundi umeme


– Msusi

– Kufanyisha watu mazoezi gym

– Kufundisha watu ujuzi ulionao

– Graphic design, mambo ya photography na videography

– Kutengeneza mikeka, viatu vya kimasai na vikapu

– Kupika keki

– Fundi seremala na watengeneza viti, makabati nk

– Fundi viatu

– Fundi cherehani

– Mwalimu wa tuition nk


Ni ujuzi gani unahisi tuuongezea hapa?

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป