Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Career Guide

Ukweli wasiokuambia kuhusu kumaliza chuo

Hongera kwa kumaliza chuo, umepata kitu kikubwa katika maisha yako.

Inatakiwa kiwe ni kipindi cha furaha kwamba umeaccomplish kitu kwenye maisha yako, ila huwa ni kipindi cha maswali yasiyo na majibu. Kipindi cha kujisikia kama hauna muelekeo kwenye maisha. Jamii inakusukuma na kutarajia makubwa kuliko wewe unavyojidhania unaweza kutimiza, macho yao sasa hayaangalia ulilolifanikisha, yanaangalia utakayoyafanikisha.

Wengi huwa na mawazo mida hii, mawazo ambayo hayana majibu, mawazo ambayo jamii inakupa ila haijui kama inakupa. Maswali ambayo wazazi na ndugu wanakufanya ujiulize ila hawajui kama wanakufanya ujiulize. Maswali ambayo unakosa majibu, maswali kama; sasa nafanya nini kuhusu hili? Niende wapi baada ya hapa? nitakuja kuwa nani? Je naweza kutimiza ndoto zangu? Na kama naweza lini?

Wakati kumaliza chuo kunatakiwa kuwe ni kuzuri, mara nyingi kwasababu ya kutokujua muelekeo baada ya hapo kunakuwaga sio kuzuri, kumejaa huzuni na mawazo, mtu unatamani uendelee tu na shule ili uendelee kuishi maisha ambayo hakuna responsibility.

Na wivu je?

Pale unapoona wenzio wanapata kazi haraka kabla yako wakati wewe umetoka kutuma cv na haujapokea majibu yoyote? au labda umetoka kwenye interview na ukakataliwa? Ukiangalia maisha yako hauoni mbele au unaona mbele yenye kushindwa, mbele ambayo haukuitegemea/ haujawahi kuitaka. Unaporudi nyumbani na kukutana na macho ya wazazi ambayo yanaelezea kila wanachowaza kuhusu wewe na kushindwa kwako kutimiza expectations zao, ya kwamba upate kazi na uanze kuingiza kipato.

READ:Kama unahisi maisha yako yanaenda taratibu

Na je vipi kuhusu expectations zako mwenyewe ambazo ulikuwa nazo kuhusu kumaliza chuo na bado hazijatimia? Vipi kuhusu kuwa na pesa, kusafiri, kuwa na nyumba na gari na baada ya miaka fulani kuingia kwenye ndoa? Na mpaka sasa wiki mbili baada ya kumaliza chuo uko na mabegi yako na simu ya mkononi haujatimiza lolote, labda wiki mbili au miaka kumi sasa haujaona kitu.

Kuhusu muelekeo wa maisha haujui barabara ipi ni sahihi, barabara ipi itakufanya upatie kwenye maisha, kiukweli hatutamani kushindwa, kiukweli hatutamani kuelekea kusikofaa ila ni njia ipi ni sahihi, njia ipi itatufanya tufike tunapotamani kwenda?
Woga wa maksi ulizopata ya kwamba labda hazitoshi kwenye kazi unayoitaka, na mawazo ya kwamba labda ungefanya vizuri zaidi ya hapo, hasa katika kipindi hiki ambacho karatasi ndio inakuwakilisha na kuonyesha uthamani wako kwenye jamii, thamani ambayo ipo hatarini kupotea maana, maana mpaka sasa unaonekana ni mzigo tena.
Vipi kuhusu urafiki, umeshazoea kuwa na marafiki kila mahali na unawaona kiurahisi ila sasa haupo nao tena na zaidi unahisi ni wachoyo na hawataki mafanikio yako kwani hawakushtui na hata wewe hauwashtui kwa kuogopa mpambano, kila mmoja amekuwa mchawi na mchoyo wa mafanikio ya mwenzie, na kiukweli sio kwamba hampendani au ni wa choyo ni mashindano, unatamani ufanikiwe kabla yao au hata wote lakini ufanikiwe.
Oh na vipi kuhusu wale wanaofanikiwa haraka baada ya kumaliza, wale wanaopata kazi baada ya kumaliza wakati wewe umesubiri na kusubiri na kusubiri lakini wapi? Unatakiwa ujisikiaje? Wivu? Hasira? Chuki?
Mawazo juu ya mawazo, usiku mwingi unakuwa macho, usiku mwingi unawaza utaitwa lini kwenye interview, unatamani kuanzisha biashara ila mtaji hauna au hautoshi, unatamani kwenda masters ila hauna uhakika unaweza kupata scholarship au matokeo hayajatoka, you are depressed.
Hauko peke yako, uko na wengi wanaopitia hali kama unayopitia wewe, kumbuka mmemaliza chuo wengi, kama unapitia hali kama hiyo, kumbuka vitu vifuatavyo:
-Ana mpango mzuri na maisha yako, anajua alikuumba kwa sababu hatoacha kusudi lake lipotee kwenye maisha yako.
– Jiunge na watu ambao mpo kwenye situation moja, katika kila kipindi kwenye maisha yako kuna wengine pia wanaopitia na wewe, kama umemaliza chuo tafuta mliomaliza nao na ujiunge nao kwenye safari hii ya pamoja, usijitenge.
– Ombea maisha yako, uko huru sasa kuna nafasi nyingi kwenye maisha yako zitakazo jitokeza, ombea mpango wa Mungu utimie.
-Ongea na watu kuhusu unavyojisikia. Usipitie crisis mwenyewe, seek help.
Don’t worry the best is yet to come. Your future is better and brighter.
Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป