Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

grayscale photography of people raising hands
Imani

Umuhimu wa kuiombea nchi yako kwa mzigo mzito

“Tanzania, Tanzania, nchi yangu naisifu, kila siku namuomba Mungu aiweke juu”

Heri ya sikukuu ya Muungano, Tanzania. Woow, Muungano, miaka 55 sasa. Bado nafikiria hekima za viongozi wetu kukaa chini na kuona umoja ni muhimu kuliko utengano, mambo yamebadilika siku hizi vijana wengi hatufikirii hivyo, tunashindana sana kuliko kushirikiana but hiyo ni blogpost ya siku nyingine.

Leo ni kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania (am yet to go to Zanzibar, na nikienda rest assured i will share a post about it). Kama unanifahamu vizuri unajua naipenda Tanzania toka moyoni, like #Tanzaniapleaseadoptme kind of love.

Lakini haikuwaga hivyo miaka yote, nakumbuka nilipokuwa secondari, Jangwani, ndipo huo upendo ulipokuja. Nakumbuka nilikuwa nachukia na nalalamika kwanini mimi ni mTZ, ambapo rafiki yangu mmoja alinishushua mpaka leo sijasahau, aliniambia “yani wewe wenzio wanalilia wawe waTZ, halafu wewe unalalmika kwanini umezaliwa TZ, shame on you”.

That day niliwaza sana, but pia that day changed my mind and my heart FOREVER. here i am, so in love with #TZ. Here i am thanking God for choosing this country for me on this side of heaven. Here i am feeling #blessed kuwa mTZ. Oh, and here i am every once in a while finding myself singing national anthem with tears in my eyes, here i am defending my country against anyone who says anything about it (i mean anything bad, you will get to see my other side), if this isn’t love, i don’t know what is?

This is why nachukia nyimbo vijana wanaimba siku hizi, kama bongo bahati mbaya and etc, bongo sio bahati mbaya, and we should stop speaking these words, we breathe negative life into them.

And so leo ningependa nikushirikishe umuhimu wa kuiombea nchi yako, what a timely post in a day like today.

Katika kusafiri kwangu nimegundua vitu mbalimbali kuhusu Tanzania nikiwa nje ya Tanzania. Unajua kama vile watu wa nje ya mahusiano yako ambavyo wanaona mazuri/ mabaya ya mahusiano yako ambayo wewe huyaoni, i got to see my country from the outsider’s eyes. Na ilikuwa ni experience iliyonifanya nijisikie kuipenda zaidi Tanzania/nijisikie kuwa nimebarikiwa kuwa mTZ, na pia nijisikie mzigo mzito wa kuiombea kwasababu kuna mazuri zaidi ambayo tunaweza kuyaachieve kama nchi.

Mistari ya Biblia kama: 2 Mambo ya Nyakati 7:14 na Yeremia 29:7, inaonyesha vile kuwa kuiombea nchi yetu ni responsibility, this is where God planted us, it is our responsibility to pray for it, like Biblical responsibility. Praying for everything, sio tu uchaguzi. Uchaguzi mara nyingi tunaomba kwasababu ya fear na kwasababu kanisa la kwanza waliomba ili Mungu awaonyeshe viongozi. Out of fear kwasababu ya kuogopa ugomvi na mapigano hasa kipindi cha uchaguzi but what if we prayed out of love miaka yote tu na sio kipindi cha uchaguzi pekee?

Kuiombea nchi kwa mzigo mzito ni moja ya sababu i believe, Mungu alitufanya tuzaliwe nchi hiyo, yes tunaiombea pia na dunia kwasababu we are still in the world, mambo yakiharibika nchi yoyote, the whole world suffers with it.

I understand mtu unaweza jiuliza naiombeaje nchi, well hilo swali ni valid, baada ya kuwa tunaombea tu amani, i am pretty sure unakuwa hauoni areas nyingine za kuiombea nchi (na sio kwamba amani sio kitu cha msingi, oh man, i have been to refugee camps i have seen the impact of wars and absence of peace in a country trust me, amani itakuwa point ya kwanza kwenye hii post).

So here are the areas i suggest we pray for:

  1. Amani- Jamani vita sio nzuri, mapigano sio mazuri na kuuana na mtu ambaye alikuwa jirani yako mliopendana kila kitu ila mkaja kupishana chama sio vizuri. Kuna mtu aliniambia hakuna vita mbaya kwenye nchi kama ya kikabila, kidini na ya kirangi (religious, tribal, ethnicity/racial). Na Tanzania tupo makabila mengi sana (120+) na watu wenye rangi mbalimbali na dini mbalimbali we need peace. Let’s pray for peace katika nchi yetu, peace in our communities, peace kwenye mikoa, peace kwenye kata, vitongoji hadi nyumba, let’s speak peace everywhere, peace, be still in the whole country.[Tweet “let’s speak peace everywhere, peace, be still in the whole country”]
  2. Afya- Afya za wananchi, afya za viongozi, every year tunapoteza watu kwasababu ya magonjwa. Ukienda hospitali yoyote ile utaona vile hali ilivyo, let’s pray for these people, our people. Tuiombee nchi yetu iwe nchi ambayo watu wanaishi mpaka wanatimiza miaka ile Mungu amewapangia kuishi (miaka ya utimilifu).
  3. Tuombee mazao ya nchi yetu/ ardhi yetu- tuombee ustawi wa mazao/mimea yetu. Tuombee ardhi iwe rutuba, kusiwe na njaa, kuwa na mvua ya kutosha katika seasons zake, tuombee hali ya hewa, tuombee our land, tuombee utalii, tuombee wanyama wetu, tuombee vyombo vyetu vya usafiri, tuombee our land and everything it is blessed with.
  4. Tuombee uchumi wetu- Value ya hela yetu (i believe in this we need to pray, and ask God to give us ideas za kuincrease value ya hela yetu but pia go to work). Nakumbuka nilipofika border ya Malawi na Tanzania nilitoa hela nyingi sana ili kupata hela ndogo ya Malawi wakati nabadilisha pesa, lakini pia hata ukiangalia value ya Euro, ama Dollar inazidi kupanda. We need to pray for the value of our money and the economy at whole, kwa maumivu kwasababu ukifanya biashara na watu wa nje itakuwa profitable hata kwako kama value ya hela yetu itapanda.
  5. Uongozi- Mungu akaweke hekima kama ya mfalme Sulemani kwenye uongozi, viongozi wanakutana na mambo mengi sana. Hata kama haujamchagua, ndio tayari ameshakua kiongozi wako. Naamini hakuna kinachotokea kwenye dunia hii kinachomshangaza Mungu, He knows it all, and so hata huyo kiongozi kuwepo God knows, basi lia mbele zake kwamba haumpendi and after that mwombe Mungu atake care of our nation, even though anayeiongoza haumpendi/haumwamini. But tuombee viongozi wote, raisi mpaka kiongozi wa familia zetu.
  6. Njaa ya Neno- Mungu aweke njaa ya kumtafuta Mungu, i believe, i personally believe nchi ikiwa na njaa ya kumtafuta Mungu hata watu wake watakuwa God- fearing na mambo mengi yatabadilika yatanyooka katika area nyingi kwasababu watu wataishi with integrity and fear of God in their lives. But pia kukiwa na njaa ya Neno wengi watakuwa reached pia in the country.
  7. Internal affairs- Hapa naongelea yale mambo yote yanayoendelea kwenye nchi, marriage, education, kazi, biashara, miundombinu, huduma za afya,za simu, za maji ets, mindset, utalii, style ya maisha na vitu vyote vinavyolijenga taifa. Kuendelea sio majengo tuu, ni mindset ya watu pia. Lakini pia sio one part of the country inajengwa vizuri na kwengine bado, let’s pray for other parts pia kuamka, let’s pray for the marriages in the country, watu wawe waaminifu. Sasa hivi Kiswahili kinaanza kufundishwa shule za South Africa that means kuendelea kwa lugha ni kuendelea kwa nchi pia, maana opportunity zitakuja sana kwasababu waTZ ndio tunajua Kiswahili sanifu. Let’s pray for all the windows and doors of heaven to open for our country, let’s pray Mungu atufungue macho waTZ tuone fursa, tuchangamkie fursa na tupate fursa. Tuombe kwamba Mungu aibariki Tanzania.[Tweet “Let’s pray for all the windows and doors of heaven to open for our country, let’s pray Mungu atufungue macho waTZ tuone fursa, tuchangamkie fursa na tupate fursa.”]

Je, kuna jambo lolote pia ungependa tuombee kwa ajili ya nchi yetu? Andika kwenye comment. Please suggest more areas, and let’s pray together for our country. Kwa vile kufanikiwa kwa nchi yetu, ndio kufanikiwa kwetu.

“Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ubariki Muungano”

Eunice.

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป