Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Urafiki chuoni | Your Guide to University Life

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Unaenda kukutana na watu wapya chuoni. Okay sio wote, kuna wale uliokuwa nao while wengine mmechaguliwa wote lakini asilimia kubwa watakuwa wapya..

That is exciting and scary at the same time.Watu wapya utakaoanza na moja kuwafahamu, utaanza upya kuwa karibu nao, utaanza kuishi nao maisha, na watakuwa kwenye memory yako. Kila ukikumbuka chuo, utakuwa unamkumbuka mtu ambaye utakutana naye sasa, unaenda kukutana naye sasa.

Urafiki chuoni, wakati naenda chuo kuna mtu aliniambia kuwa,’ watu unaokutana nao chuo unaweza dumu nao muda mrefu kwenye maisha, kwasababu mmekutana nao kipindi uko kwenye the most defining time of your life’Lakini pia kama vile mambo mengine kwenye maisha yalivyo na mwanzo na mwisho sometimes pia unaisha urafiki.

Chuoni kuna urafiki wa aina tatu:

– Urafiki kutokana na kwamba mpo sehemu moja ie mpo course moja, group moja La assignment, room moja hostel nk

– Urafiki kutokana na kwamba mnapenda vitu sawa ie mnakutana club kwahiyo mnashtuana kwenda, mnasali pamoja, mnacheza sports

– Urafiki kutokana na kwamba mmeamua kuwa marafiki na kuwa there for each other.Aim for the last one, because that one will last.

Nilikuwa na marafiki wengi chuo, waliodumu ni wale nilikuwa nimeweka uamuzi kua nataka wawe kwenye maisha yangu, we all need people around us. Marafiki ni familia unayoichagua.

Chagua wisely.
Amua watu unaotaka wadumu na invest in that friendship. Invest in it.

Amua watu unaotaka wakae kwenye maisha yako, and let them know that is what you want. It is important if they feel the same way, ili urafiki usiwe wa upande wako pekee.

Naamini utapata marafiki wapya, wachague wale unaoona wanaelekea kule unatamani maisha yako yaelekee.
Ukimaliza chuo, you can look back and see that you don’t have regrets.Now that unaenda, you have a chance to build a regret free life.
Who are you choosing????

Eunice

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »