Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Random

Maswali ya kujiuliza kabla haujaingia kwenye siasa

Watu wengi huingia kwenye siasa kwasababu ya cheo & pesa. Wengi huwa hawaingii kwa nia ya kuwatumikia wananchi, kulitumikia taifa, wanaingia kujichumia ya kwao na kufuta jasho walilotokwa kipindi cha kampeni. Ndio maana mgombea akishapata cheo hasikilizi wananchi, anawadharau tena. Cheo & Pesa.

Nchi zetu nyingi za Afrika ni changa sana, wengi toka tupate uhuru hata miaka 60 hatujafikisha, kuna maeneo mengi sana ya kuyaboresha ili tuendelee. Sio lazima uingie kwenye siasa ili ulete maendeleo, sekta ziko nyingi, cha msingi ni uwe mwaminifu, ufanye kwa ubunifu na juhudi sekta uliopo na ufanye mabadiliko chanya hapo hata ukiondoka mwingine ataendeleza ulipoishia. Kila mtu kwa sekta aliyopo inabidi ajiulize, ‘ninaifanyia nini nchi yangu?’ ‘ninatumiaje maarifa niliyonayo, nguvu na hekima kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yangu kupitia hii sekta niliyopo?’.

Pia Soma : Kwanini waAfrika tunatabia ya kujidharau?

Nakumbuka niliwahi kuambiwa kuwa kusudi lako sio lazima kiwe kitu kikubwa ukajulikana hatari, kusudi lako linaweza kuwa tu ni kuzuia pesa zisiibiwe sehemu fulani, na hivyo ukawa umechangia kwenye nchi kwa namna hiyo. Kumbuka kuwa kwenye maisha tunaathiriana, hivyo fikiria picha kubwa zaidi.

Unapenda kufanya kitu gani, fanya hicho na endeleza hiyo sekta kwa ubora, ukiwa mwigizaji halafu ukaiendeleza sanaa ya uigizaji ya bongo tukawa tunapenda filamu zetu na zikapendwa na wengine kama vile filamu za korea zilivyosasa tayari umefanya maendeleo. Ukiwa mchoraji, chochote kile unachopenda kufanya ndio kinaweza kuwa kitu ulichotakiwa kuchangia katika maendeleo ya nchi, kuna sekta nyingi.

Narudia tena sio lazima kila mtu awe mwanasiasa ili kuleta maendeleo, ila kama unajisikia kuitwa huko, utaifanyia nini nchi yako? Na kweli unapenda siasa kwaajili ya kuwatumikia wananchi au pesa & cheo?

Nawasilisha mawazo yangu, niambie yako kwenye comment.

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate »