Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku

Kama Unafikiria Kujiua…

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa saba, mwezi ambao ulikuwa mgumu sana kwangu.

Nakumbuka kuna siku tulikaa sebuleni, nikamwangalia mama na kuwaza, ‘hivi nikijua, kuna mtu yoyote atakayejali?’.

Nakumbuka tena usiku mwingine, tulimaliza kula na wote wakaelekea kulala Ila Mimi nilikuwa nimebaki sebuleni, nikiangalia feni na wazo likanipitia,’ hivi nikiweka khanga kwenye feni, itaweza kunibeba mpaka nijiue? Au ndo feni itaanguka na hivyo nitashindwa kujiua?’

Na katika wakati ule ndio nikagundua kuwa nahitaji msaada, nahitaji kuongea na mtu, napitia wakati mgumu ambao nahitaji kuongea na mtu ili mzigo upungue moyoni.

Nilikuwa napata wakati mgumu kupata kazi, na kujua jinsi ya kuishi maisha ya mtaani bila hela, na bila sehemu ya kwenda kila siku nikiamka.

Nilikuwa kipindi cha Giza kwangu, sikuwa na amani, furaha wala sikujisikia raha ya chochote.

Kila siku nilikuwa bora ya Jana.

Siku chache baadae mtoto wa jirani yangu alijinyonga, alikuwa ni kijana wa umri wangu.

Niliona huzuni ilivyotanda kwenye familia yake na mtaa wake.

Niliona maswali na kuchanganyikiwa kwa mama yake.

Niliona jinsi tulivyompoteza jirani lakini pia familia ilivyompoteza mtoto wao wa kiume.

Alijiua na kutuacha na maswali.

Alijiua na kutuacha na huzuni ambayo yeye alidhani anaimaliza kwa kujiua.

Kujiua kwake kulifukia wema wote ambao ungekuja kutokea huko mbeleni baada ya jambo ambalo alikuwa analipitia kupita.

Mambo mazuri yote na ndoto zake zilikufa pamoja naye.

Nilipata kuona jinsi mama yake alivyoteseka, akijiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake na kila mtu mtaani kujisikia kama hana msaada kwasababu labda kama angeongea tungeweza kuwa wa msaada kwake. Lakini, it was too late.

Naelewa unavyojisikia sasa, nimeshajisikia hivyo pia. Nimeshapitia kipindi ambacho hauoni mwanga, hauoni tumaini, unachokiona ni mwisho, unachokiona ni giza nene usiloluja linaisha lini.Kuna muda maisha yanakuwa magumu sana, kuna muda unapitia mambo magumu na hauoni mwisho wa hilo gumu ukifika mapema.

Unakosa amani, tumaini, furaha na ukiangalia watu wote duniani, ni kama hawasikii kilio chako, ni kama hawaoni machozi yako.

Unajihisi uko peke yako, unajihisi umetengwa na unahisi hautokuja kuwa na furaha tena.

Na unahisi njia peke ya kumaliza hali hiyo ni kujiua.

Kama unafikiria kujiua, ningependa nikwambie mambo ambayo nilitamani nimwambie kijana aliyetutoka mtaani kwetu:-

—++Magumu yanapita, maisha ni mzunguko wa mazuri na mabaya. Mapito huwa yanapita.

-++-Ongea na mtu kuhusu jinsi unavyojisikia, tumewekwa kwenye dunia wengi kwasababu hakuna anayejitosheleza mwenyewe. Utashangaa vile watu wanapenda kuwa wa msaada kwako, wape nafasi.

-++- Ukijiua unaondoa maumivu unayoyasikia na kuwaachia wale unaowapenda. Ukiongea unapata msaada na watu wakukupunguzia mzigo kwani na wao wataubeba pamoja nawe.

–++Wewe ni wa muhimu sana, umewekwa duniani kwa kusudi na jaribu halijawahi kumpata mtu likiwa nje ya uwezo wake, Mungu anajua unaliweza hili na utalishinda hili.

–++Kwasasa unaweza dhani hakuna anayekupenda, wakati ukiwa katika mawazo hayo Mara nyingi utaamini haupendwi na umpweke, lakini ukweli ni kuwa unapendwa, we we ni wa thamani kwa watu wako wakaribu.

–++Unafuture huko mbeleni, ambayo hautaweza kuiona ukiondoka sasa. Neno linasema kwenye Yeremia 29:11, kwamba mawazo anayokuwazia Mungu ni mema, usijiue upate kushuhudia na kusimulia.

Kujiua ni uamuzi permanent kwa tatizo ambalo lipo temporary, utajisikia tena furaha, amani na raha maishani. Maisha ni safari.

(Kama unataka mtu wa kuongea nae, nicheck kwa email – hie@abiblegirl.com)

(Kuna hii website unaweza kuitembelea, inaposti vitu vinavyoweza kukusaidia kama una mawazo ya kujiua, stress au msongo wa mawazo, imenisaidia Mimi pia, natumaini itakusaidia nawe – Recklessly Alive)

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป