Happy Valentine’s day msomaji wangu, ni matumaini yangu unaifurahia Valentine’s day kama una mpenzi au hauna, kwasababu hata kama unaye bado unawatu wanaokupenda na kama hauna bado una ndugu, jamaa na marafiki wanaokupenda pia.

Kama uko chuoni na unatamani kusherehekea Valentine’s, hii hapa ni list ya mambo mbalimbali unayoweza kufanya na mpenzi au marafiki zako kwenye siku hii ya wapendanao:


Kuangalia movie pamoja

Kula chakula pamoja

Kutoka out (kutembea/ kwenda museum/ au vivutio vyovyote vilivyopo sehemu ulipo/kwenda beach)

Kupeana zawadi (kubadilishana, mimi nilikuwa nampa room mate wangu na yeye ananipa zawadi)

Kuandikiana barua za jinsi huyo mtu anavyogusa maisha yako

Soma Makala Inayoendana : Jinsi ya kuwa Mpenzi Bora

Kujitengenezea utamaduni wa kusherehekea (mimi nilikuwa najinunulia chipsi mayai na kusoma kitabu siku hiyo)

Kutumia siku hiyo kupumzisha akili na ubusy wa masomo.

Kuwapigia nyumbani na kuwaonesha upendo kwa kuwaambia jinsi unavyowapenda.

Kutumia siku yako kwa kushinda kwa wale wanaokaa off campus na kupiga nao stori (Mnaweza mkapika na mkala pamoja au kama uko off ukawakaribisha marafiki zako wanaokaa hostel waje kula kwako)

Kufanya party ya room (Kununua chakula pamoja na kula kama wanaroom)

Jiandikie barua mwenyewe ya jinsi gani unavyojipenda, vitu gani unavuoenda kutoka kwako na unajihadi kujipenda kwa namna ipi kuanzia leo (self love)


Na hizo ni ideas 11 za jinsi unavyoweza kusherehekea Valentine’s day ukiwa chuo.

Je, umepanga kusherehekeaje Valentine’s day mwaka huu?

Eunice

You May Also Like

4 thoughts on “Jinsi ya kusherehekea Valentine’s day ukiwa chuoni | 11 Ideas

 1. Rebeca

  Wow nzuri dear

  1. Eunice Tossy

   Asante sana Rebecca.

   Asante sana kwa kusoma pia.

   Happy Valentine’s day dear, unasherehekeaje leo?

 2. Jose B

  Mbele ya UE hiii kupumzsha akili ni ngumu

  1. Eunice Tossy

   Ni kweli.. naelewa.

Share Your Thoughts With Me

Translate »