Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

islamic african american female in hijab on sofa with notebook
Maisha ya Chuo,  Vitabu

Vitabu 5 ambavyo kila mwanachuo anabidi avisome akiwa chuoni

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Likija kenye swala zima la kuwa chuoni, kuna wengine wanakuwa na mud mwingigi huru kutokana na kozi zao na wengine wanabanwa sana, lakini ikija kwenye swala la maendeleo binafsi au kujiandaa na maisha ya mtaani wote wanatakiwa wajiandae, wawe na nana ya kuona dunia na kujiona wao kitofuti a kwa njia chanya hata kama muda unawabana wengine kufanya mambo ya maendeleo binafsi.

Kama ni mwanachuo unayependa maendeleo binafsi na kuiona dunia kwa jicho la tofauti ukiwa bado uko chu vitabu hivi vitano ni vya muhimu kuvisoma;

= The third door cha Alex Banayan

Kitabu hiki kinaweza badilisha vile unahisi mafanikio yalivyo. Wengi huwa tunahisi kuna barabaraba moja ya mafanikio aliyeandika kitabu hiki anasema kuwa kuna mlango wa tatu ambao wengine huwa hawauoni ila wengine wachache hufanikiwa kupitia huo.

= 101 secrets for your twenties cha Paul Angone

Hiki kitabu kina mambo ambayo mwandishi ameyaandika ambao ni ukweli mchungu ambao ni mzuri kwa kila aliye na miaka 20+ kuyajua. Kwa vile mwanachuo uko umir huo, ni vizuri ukijua mapema.

= The defining decade cha Dr Meg Jay

Kuna ule msemo maarufu watu husemaga kuwa ’30 is the new 20′, kwenye kitabu hiki mwanasaikolojia huyu anaukataa huo msemo na kuonyesha ni jinsi gani na maeneo gani ambayo miaka yako ya 20 inabidi uyafanyie maandalizi na uyaangalie kwa makini maana ukipotezea unaweza haribu miaka yako ya 30 au hata maisha yako ya huko mbeleni.

= How to become a straight-A student cha Cal Newport

Siri ya kufaulu sio kusoma sana, ni kusoma kijanja. Kwenye kitabu hiki mwandishi anashea siri za kusoma kijanja ambao wanafunzi waliopo mavyuoni waaopataga A wamezitumia kupata A zote.

Pia Soma : 7 Books to read when you feel like a failure

= 52 cups of coffee cha Megan Gebhart

Kwenye kitabu hiki mwandishi ameongea na waanzilishi na viongozi wa kampuni mbalimbali ambao waneshea hekima za maisha na vitu walivyojifunza kwenye maisha yao. Najua umri wetu wengi wetu tunahisi maisha ni mashindano ila kitabu hiki kina hekima mbalimbali za maisha kutoka kwa waliotuzidi umri, walioishi kwa muda mrefu na kufanya mengi zaidi yetu. Ni muhimu kupata hekima hizi mapema.

Eunice

One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป