Download Mwanachuo planner ili uandike malengo yako ya chuo sasa

Life Tips

Vitu 10 vijana wanapaswa kuanza kuvifanya mapema kwenye maisha yao.

Reading Time: 2 minutes

Karibu tena kwenye blog yangu, natumai umejiandaa kuanza vyema Juni. Kama bado haujapata planner ya bure kabisa ninayotuma, unaweza kusubscribe lwo ili kuipata. Na kama umeipata, naomba mrejesho wako, na kama kuna vitu vya kuongezea ungependa viwepo niambie iliniongeze kwaajili ya mwezi wa saba

Leo, napenda niongelee mambo machache ninayoyaona ni muhimu kwa vijana kuanza kuyafanya mapema, mapema kabisa nikimaanisha sasa.

1)Kumjua Mungu kwa kusoma Neno lake.

Kiukweli vijana tuna majaribu mengi sana yanayotuzunguka na kuna uvivu mwingi unaotuzunguka. Leo nimeamka nikaanza kuangalia movie ya Kikorea badala ya kusoma Neno na kukua Kiroho. Lakini naamini hiki ndicho kipindi ambacho tuna nguvu, na uwezo wa kumjua Mungu kirahisi. Tuna nguvu za kufunga, tuna nguvu za kusoma Neno, kuhudumu nk

2) Kujifunza /Kuthubutu mambo mbalimbali

Mimi naamini katika kujifunza vitu mbalimbali, unaweza ukaona hakuna umuhimu Leo, lakini huwezi jua umuhimu wake miaka ijayo, kuthubutu kuna kusaidia kujua kama hili swala linanifaa ama halinifai kwenye maisha yangu.

3)Kunywa maji

Nimekutana na watu wengi wanaoshangaa ninavyotembea na chupa ya maji kila mahali, na ingawa naonekana nafanya kitu cha muhimu sana kiafya, I promise sifuatilii mambo yote madokta wanasema. With that being said, naona kunywa maji na kufanya mazoezi ndio mambo pekee ya kiafya ninayofanya. Kama ni kweli mwili wa binadamu unatengenezwa na 50-75% ya maji (Google??), then kunywa maji ni jambo la muhimu sana. Kwangu natumia kama kunywa maji ni njia rahisi ya kujisafisha mwili, unapoenda haja ndogo unausafisha mwili, lakini pia kwa wale wanaopenda urembo ngozi inatakata.

4) Kufanya mazoezi

Mi napenda tu kukimbia, nimejaribu gym ila naona kama ni tabu sana. Nahisi mazoezi yaliwekwa ili kila siku tuufanyishe mwili kazi, and so najaribu kuenjoy wakati nafanya mazoezi. Hivyo huwa napenda kukimbia wakati wa asubuhi ili nione sunrise au jioni nione sunset + nakuwa na music napumzika from time to time. Mazoezi sio lazima yawe mateso, you can even do dancing tu. Unajua tuna mwili mmoja tu hapa duniani.

5)Kusave hela

Najua ujanani kuna majaribu mengi, na pia kuna vitu vingi tunavyovienjoy kufanya ambavyo ni vya gharama kwetu. My mentor ananishauligi sana hili swala, pamoja na pastor Sam analiongeleaga sana kwenye Weekend Worship, vijana kusave hela hata kidogo kidogo inakusaidia kwenye maisha yako. Najua wengi tumekulia kwenye familia zinazosubiria mshahara mpaka mshahara na hivyo tabia ya kusave hela hatujaiona ikionyweshwa kwa mifano, but ni vitu vya kujifunza. Unaweza kusave hata tu ya kuitoa msaada sehemu, ya kusafiria au ya kukusaidia huko mbeleni kwenye maisha yako.

6)Kuchukua mapumziko ya mitandao ya kijamii

Soma: Kwanini niliacha kutumia mitandao ya kijamii

Najua unahisi ukitoka kwa muda social media, utakuwa nyuma au dunia itasimama, ila ukweli ni kuwa unahitaji break hiyo kwaajili ya afya yako.

7) Kusoma vitabu

Kuna faida nyingi za kusoma vitabu, moja wapo in kukupa maarifa mapya na kupanua dunia yako .

8) Kuacha mawazo na kupumzika

Kama vijana kuwaza sana, na kuwa na stress za maisha inatuumiza sana kuliko kutusaidia. Kila kitu kitakuwa poa in time.. We all don’t know what we are doing with life, I promise.

9) Kutengeneza connection na mahusiano na watu

Kuna umuhimu wa kutengeneza mahusiano ya watu watakaokumentor, lakini pia marafiki utakao kuwa nao kwenye safari ya maisha. Kuna msemo unasema ukitaka kwenda haraka,nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako.

Soma: Kwanini vijana wengi hushindwa kwenye maisha

10) Kuacha kujilinganisha na kupata experience kikazi

Vijana wengi tunajiumiza kwa kujilinganisha na watu waliotutangulia au tulionao sawa tukisahau kila mtu anasafari yake ya maisha. Lakini pia muda huu was ujana ambapo tunanguvu ndio muda was kugain experience katika mambo mbalimbali na hivyo kugain wisdom kwenye maisha.

Eunice

6 Comments

Share Your Thoughts With Me