Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Vitu 5 vitakavyokusaidia kutozama kwenye huzuni nyingi na mawazo ya ugumu wa maisha

Sijui ni mimi tu au na wewe pia unajisikia hivi, ila mimi nahisi sio kwamba nilidanganywa, ila hakuna aliyewahi kuniambia ukweli kuhusu maisha ya duniani, yani ukweli kuhusu kuwa mtu mzima na maisha ya duniani yalivyo, ule ukweli halisi. Najua tunapokuwa watoto wazazi wanajitahidi kutulinda tusijue hata kama wana mawazo kwa kuwa hawana ada, ila unapokuwa mtu mzima na unakutana na gharama hizi unakuwa hujui jinsi ya kudili na ile huruma kwa wazazi wako baada ya kujua kuwa kumbe wazazi wako walipitia mengi lakini pia hujui cha kufanya na ile huzuni ya utafutaji na kutokujua kuhusu upataji na gharama za maisha. Sio hayo tu lakini maisha yana mambo mengi kama binadamu wengine pia, tunaona na tunahuzunika na yanayoendelea kwetu, kwa ndugu zetu, kwa wananchi wenzetu nk, mazingira yetu pia yana vitu vingi sana vya kuhuzunisha ambavyo kama mtu mzima unayeelewa maisha yanakufanya uumie na uwaze. Yote haya huleta huzuni na mawazo na hata kupelekea sonona.

Kwenye hii makala ningependa nikushirikishe vitu 5 ambavyo vinaweza kukusaidia kutozama kwenye dimbwi la mawazo na sonona kila siku hasa likija swala la yale tunayoyapitia duniani na wanayopitia wengine, njia hizo ni;

  • Kujua na kukubali kuwa maisha yana mabaya na mazuri, magumu na mepesi

Vitu vingi hututesa kwasababu huwa tunachelewa au tunakataa kukubali. Kukubali ukweli kuwa maisha ni magumu, maisha ni mepesi, maisha yana mabaya lakini pia maisha yana mazuri. Ukweli kuwa kuishi duniani ni jambo la furaha, lakini pia ni jambo la huzuni, dunia ni nzuri lakini pia dunia ni mbaya. Dunia hii hii ina mvua inayokusaidia kupata mazao, dunia hii hii ina mafuriko yanayochukua uhai wa watu na kuharibu makazi yao.

Muda mwingi huwa hatufikirii kuwa jambo fulani linaweza kutupata kama binadamu chini ya jua, ila ukweli ni kuwa kwa kuwa chini ya hili jua, hisia, matatizo na mazuri yanayowapata wengine yanaweza kutupata na sisi, hiyo ndio maana ya kuwa binadamu, utapata hisia za kibinadamu, utapitia mambo ambayo binadamu hupitia. Inawezekana sio yote na ndio maana huwa tunahisi sisi hayawezi kutupata ila yanapokukuta kubali, haraka sana, husaidia sana kutoumizwa na hilo jambo kwa muda mrefu au kwa maisha yako yote. Unapokubali ndio akili unaweza kuifikirisha kuhusu cha kufanya kama suluhisho.

Bonyeza hapa kusoma makala hii kama unahisi umechelewa kwenye maisha

  • Thamini mchango wako duniani kwa namna ile unayochangia

Hakuna mtu ambaye maisha yake hayana maana kwenye dunia, unaweza hisi hauna mchango lakini familia yako inakutegemea na bila uwepo wako mambo hayaendi, au bila uwepo wako kwa marafiki zako mambo hayaendi nk.. Kama ni mwalimu, jali na thamini mchango wako huo kwa wanafunzi wako. Hii hukufanya uone umuhimu wa maisha yako duniani katika hali yoyote ile unayoipitia na linaweza kukuhamasisha unapopitia magumu kuyashinda kwaajili ya hao wanaokutegemea au kuyashinda ili kuendelea kutoa mchango wako vile unavyochangia duniani.

Bonyeza hapa kusoma makala hii kama unafikiria kujiua

  • Jua maisha hayana jambo linalodumu milele

Raha ya kuishi ni kuwa maisha hayana jambo linalodumu milele, si shida, si raha. Kuna kuwaga na misimu, msimu wa furaha, msimu wa huzuni nk. Binadamu tunapenda kuwa na furaha siku zote maisha ambayo sio uhalisia wa jinsi maisha yalivyo lakini pia hayakusaidii kukua, lakini pia hauwezi kupitia shida kila siku zitakuchosha. Ingawa hali halisi ya maisha iko hivi ila ni ubinadamu kuhisi kuwa tunapitia shida tu maana hisia hasi hutuumiza sana na tunazikumbuka sana. Kwa ugumu wa maisha ni muhimu kujikumbusha kuwa hayatokuwa magumu milele. Ni muhimu kujikumbusha kuwa mazuri pia yapo, hilo unalopitia sio la milele, jikumbushe hili kwa wakati wote. Kwenye maisha ni kuna uzuri na ubaya pia, unapopitia ubaya jua uzuri unakuja, jua ubaya haudumu lakini haimaanishi uache kuishi kwasababu ya ubaya. Ikifika wakati ukaona hilo unalopitia ndio mwisho au hiyo hali uliyonayo ndio utakuwa nayo milele ndio unakuwa mwisho wako maana unakuwa hauna nguvu ya kuendelea kupambana au kufikiria kuhusu mambo ya kufanya kujitoa kwenye hali hiyo.

Bonyeza hapa, kusoma hii kujua jinsi ya kuinyamazisha sauti hasi iliyoko ndani yako

  • Fanya mazoezi, jaribu kucontrol yale unayoweza kucontrol

Kufanya mazoezi hukufanya kwa wakati ule kufikiria jambo lingine na sio matatizo yako. Kufanya mazoezi hukufanya kucontol jambo unaloweza kucontrol, huusaidia mwili wako kujisikia vizuri. Jitahidi kucontrol yale unayoweza kwenye maisha, yale usiyoweza yaachilie. Maoezi husaidia sana kwenye afya yako ya akili na ya mwili.

-have a good time, nenda nature, kaa na marafiki na msiongelee tu matatizo

  • Furahia maisha na kuishi

Jitahidi kwenda kwenye uota wa asili, kuwaangalia wanyama, vipepeo nk. Furahia kuwa hai, tafuta furaha kwenye ladha tamu za vyakula, filamu nzuri, kucheka na marafiki, kwenye mziki nk. Sio kila muda unaweza kuwaza matatizo au kulalamikia maisha, maisha yana mengi zaidi ya hilo tatizo moja, tafuta furaha kwenye kuishi, kwenye maisha, kwenye kicheko cha mtu unayempenda, furahia upole na ukarimu ambao mtu usiyemjua anakufanyia, ni kweli watu wanaweza fanya mabaya lakini kwa wakati huo kuna mtu anakufanyia wema na hayo nayo ni maisha, furahia hilo. Furahia kuishi, kuwa hai kwa kujifunza vitu vipya, kucheka na watoto wako nk nk. Hakikisha hauumizwi tu kwenye maisha ila pia unafurahia kuwa hai na kufurahia na kukumbuka mazuri yake pia.

Pia Soma : Mambo ya kufanya unaposalitiwa na mpenzi wako

Haya yote naongea sio kwa kusema kuwa nakataa ugumu wa maisha haupo, upo na sio kwamba vitu hivi vitaondoa hali ngumu hiyo, hapana. Ila labda vinawea kukusaidia kudili navyo, vinaweza kukusaidia usizame kwenye dimbwi la huzuni na sonona, vinaweza kukusaidia usiwe kwenye hali mbaya wakati wote lakini uendelee kupigana kwaajili ya maisha yako na kutafuta furaha na uzuri kwenye maisha yako.

Eunice


Kama ungependa kujiunga group langu la WhatsApp ambalo natuma makala hizi moja kwa moja, BONYEZA HAPA.

Na pia kama unapenda kusapoti uendeshwaji wa blogu hii kifedha, unaweza nisapoti kwa kutuma kiwango chochote utakachopenda kwenda namba hii 0627975502. Fedha hizi zinanisaidia kulipia hosting ya blogu hii na pia vocha kwaajili ya mabundle ili kuweka maudhui hapa. Asante sana

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป