Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya kila siku

Unautumia vipi wakati wako?

Tangu utotoni sijawahi kuiona Jumatatu au Jumanne imebadilika?!

Muda hauendi ni sisi ndio tunaoenda

Nimetolea tu mfano wa hizo siku mbili kujaribu kukuonyesha kuwa siku zipo vile vile kama kanuni hazibadiliki.

Mama yangu aliniambia kuwa nilizaliwa jioni siku yaJumanne tarehe 14, mwezi Novemba mwaka 1995.

Ingawa nilikua sijitambui nina uhakika jumanne iliyofuata sikuwa vilevile kama nilivyozaliwa

Nimepitia mabadiliko ya ukuaji hatua kwa hatua na mpaka leo hii ni binti nimemaliza chuo kikuu jambo ambalo sikuwahi kudhani lingetokea haraka hivi

Kwa wale walio kwenye hatua kama yangu tujiulize hili

Ni kipi hasa nimefanya kwenye maisha haya???

Kinachotisha zaidi ni kwamba huu muda ambao wengi tunausubiri ili tufanye vitu fulani wenyewe upo tu yani mithili ya bidhaa iliyowekwa sokoni ikiwa na tarehe ya kuisha ubora wake

Siku ikifika bidhaa itaondoka sokoni na tarehe hiyo hiyo itaingizwa bidhaa nyingine mpya

 

Hapo umeelewa ni nini namaanisha, muda ni namba zinazobadilika tu na zikifika mwisho zinajirudia tena

Nawaza kwa sauti siwezi kuukomoa muda kwa kusema unaenda kwani wenyewe upo tu huku nikijitazama mimi ndio naenda hivyo

Unautumiaje wakati wako???(simaanishi muda ambao wengi tunausubiri ila wakati wako wa kuishi wewe kama kijana ukiwa na nguvu).

Kuna kitabu nasoma ambacho kinaelezea kanuni ya 18 /40/20 kwamba tunapokua kwenye rika hili wengi huwa tunajali hivi nikifanya hiki watanionaje, ukifika miaka 40 hatutajali tena watanionaje na inapofikia miaka 60 utagundua kumbe hakukua na anaekufikiria.

Swali ni moja tu, Unautumia vipi wakati? wacha kusema nina NDOTO lakini….!!!

MUDA HAUENDI NI SISI NDIO TUNAENDA


Imeandikwa na Christine Bellington

Blogu yake ni : Embrace Tanzanian Youth

Unaweza kumpata Instagram na Facebook


Makala nyingine iliyoandikwa na Christine Bellington

Kuoa na Kuolewa ni sehemu ya kutimiza kusudi lako

Know the facts, but understand your truth


One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate »