Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku

Kwanini wanawake hawapendani?

Wanawake…

Ushawahi kuwa mwanafunzi halafu ukawa una makosa kila siku shuleni.. Mpaka ukawa unajiuliza kwanini Mimi?

Nahisi wanawake ni kama huyo mwanafunzi. Maana mengi ambayo ni mabaya kwenye dunia huwa inasemekana ni wanawake waliosababisha.

Au labda, ni Mimi tu ndo huwa nafikiria hivi..

Mi pia ni mwanamke..

Anyway, inajulikana na imesambaa kwamba wanawake hawapendani.

Yani kwamba unaweza panda kwenye gari halafu mwanamke mwenzio akakunyali bila sababu.

Na hata haumjui.

Wanawake wanachukiana.

Inawezekana pia sio kwamba hatupendani Ila kwasababu tayari inajulikana kuwa hatupendani, automatically unakuwa unaishi kama vile mambo yanavyojulikana… Hii inaitwa Stereotype threat.

Lakini nisiwe mtu chanya sana mpaka nikawa sioni mambo yanayoendelea, watu husema adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie. Lakini niseme pia siku hizi wanawake wanajitahidi kusimama na kusupport wanawake wenzao. Vyote vipo, vyote vinaishi kwa pamoja.

Ila kwa vile topic yangu sio sababu za upendo ila sababu ninazohisi za kukosekana upendo basi naomba nisiongelee lolote chanya, ingawa kwa experience yangu Mimi mengi ni chanya..


Naomba niongee kuhusu mdada aliyeenda kwenye interview, akapita, ila kwa vile boss wajuu ni mdada akambania nafasi, na akashindwa kupata kazi kwasababu hiyo.

Naomba niongee kuhusu mdada aliyesambaziwa mambo yake ya ndani na mdada mwenzie ili kumdhalilisha.

Naomba niongee kuhusu mdada anayeshindana na mdada mwengine ili aonekane yeye ni bora kuliko mwenzie.

Naomba niongeee kuhusu mdada anayemshusha thamani mwengine akidhani huko kuna mpandisha yeye.

Naomba niongee kuhusu mdada anayejisikia kutishika akimuona mdada mwengine mbele yake. Kwani anamuona mtu wa kushindana naye, kwa urembo, urefu, hela, boyfriend mzuri, kuolewa nk

Naomba niongee kuhusu mdada anayetamani kuwa peke yake kwenye magroup ya wanaume, ili awe mrembo peke yake, aonekane yeye, lakini pia hana marafiki wa kike kwasababu wanawake ni wanafiki, wanawake ni wambeya, wanawake sio watu wazuri, haendani na wanawake wengine.


Ipo shida kwenye namna wanawake wengi tumekuzwa kuiona dunia, na kuwaona wanawake wenzetu

Jamii inatupima kwenye vitu ambavyo vinatushusha na kuona kuwa inabidi tuwe bora kwenye hivyo.. Mfano mashindano ya urembo.

Kiukweli sioni point yake, na kwa vile kila mtu ni mfano wa Mungu na ni mrembo, bado huwa tunajiona hatujafikia uwezo, na hatuwezi kufikia kwasababu kila mtu ni mzuri. Na ndio maana kuna kuwa na wivu, kwasababu ukimuona mwanamke mwingine unamuona bora kuliko wewe. Unamwangalia juu hadi chini kujua kipi umemzidi au kipi amekuzidi katika mashindano uliyojiwekea/au uliyowekewa na jamii, ukiaamini maisha ndivyo yalivyo. Au kila mtu anafanya, ni kawaida…. Stereotype threat

Kuna nafasi ya mtu mmoja juu, na ni lazima niwe Mimi.

Kuna vile wanawake wengi tunategemewa kuwa katika level fulani, kazi fulani, au eneo fulani. Idea ya kwamba kuna wanawake wafanyakazi, sehemu ambayo maboss ni wanaume karibia wote, inaleta wivu na mashindano.. Unatamani upande ngazi lakini kwa vile tumekuzwa na jamii ambayo nafasi hizi huwa za wanaume, mwanamke utakayechukua nafasi hiyo utakuwa mmoja wa wengi… Utakuwa umechukua ile nafasi inayogombaniwa na wengi.

Na kwa vile tunategemea mtakuwa wachache, hautohangaika kumpandisha mwanamke mwingine, kwasababu anaweza kuchukua nafasi yako. Na hii ndio sababu nahisi kuna mashindano kati ya wanawake ofisini, na kuna wivu na wachache waliojuu ambao hawafanyi chochote kupandisha wengine.

Tuwalaumu hao wachache?

Hapana.

Adui wa mwanamke sio mwanamke mwenzie, ni mindset tuliyokuzwa nayo.

Inayotufanya tuone maisha kwetu ni maishindano, ya urembo, kupigania wanaume kwa vile tumeambiwa ni wachache na ni lazima umpate ili uonekane umefanikiwa kwenye jamii, kwasababu pia usipoolewa ni unaonekana umefeli. Survival of the fittest.

Muda umefika kwa wanawake kuona kuwa mtu pekee anayekuelewa kwa undani ni yule anayepitia safari sawa na we we, naye ni mwanamke mwenzio.

Mwanamke mwenzio sio adui yako.. Kuna nafasi ya kila mmoja wetu kupanda, maisha sio mashindano.

Tuungane kwa pamoja kuzipiga chini ideas za jamii zinazolenga kutudidimiza, kutufanya tuonane kama washindani, na tuchukiane.. A nation divided is a nation conquered.. A gender divided is a gender conquered..

Tukikaa chini kufikiria sisi sote tuko sawa, na kuna nafasi ya kila mmoja wetu kuwa pale Mungu alimwandikia awepo, tuungane tusimame kwa pamoja, tusukumane ili kufikia malengo yetu.

Umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu.

Eunice

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป