Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Imani

Mungu, kwanini Mimi?

Chukua sekunde 30 kufikiria future yako.

3⃣0⃣

Umeona nini? Umejiwazia yapi? Unajionaje huko mbeleni?

Leo asubuhi nimeamka nakufanya hilo zoezi, na ukweli ni kwamba nimejiona mbali, nikifanya makubwa, na mazuri.

Mpaka nilipowaza kuwa labda hii ndio inanisababishia msongo wa mawazo na stress.

Hakuna hata wakati mmoja ambao nimewaza kuhusu future yangu, na nikawaza na challenges au matatizo nitakayoyapitia. Wakati kiukweli maisha yana mazuri na magumu, na hata future yangu pia itakuwa na mazuri na challenges.

Siko kinyume na watu kutamani kufika sehemu fulani, lakini nipo kinyume na watu kuamini kuwa kwakuwa ni wakristo na tumebarikiwa basi future yetu itakuwa nzuri bila matatizo.

Kuamini kuwa matatizo ni ya watu wasio mwamini Mungu.

Kupitia wakati mgumu ni kwa wenye dhambi tu.

Kupitia shida ni kwa wasio na imani.

Na ukiwa na hali ngumu ya maisha kuwa imani yako ni ndogo, umetenda dhambi au haumuamini Mungu vizuri.

Kwaaina Fulani, naona mahusiano yetu na Mungu yamekuwa ya ‘nipe nikupe’. Ya kwamba nitakuwa mwema, na wewe utanifanyia mema, na ndio maana mabaya yakitokea tunaona Mungu ametuacha, au tunahisi tumetenda dhambi au pia tunahisi Mungu hayupo.

Mwaka huu umekuwa mwaka mgumu sana kwangu, umekuwa mwaka wa mabadiliko sana kwangu katika maeneo mengi, nimekuwa napitia magumu si mimi tu Ila hata watu wakaribu yangu pia, nimejiuliza maswali, nikachoka moyoni, nikajaribu kutafuta amani, nikavunjwa moyo na mengine mengi ambayo yanatokea kwavile tunaendelea kuishi duniani.

Nimemaliza chuo mwaka Jana, na kwavile ni mkristo na Nina imani nilikuwa naamini ni haki yangu kupata sehemu fulani kazi, na kwavile nimekaa naona sijapata, nikaanza kujiuliza au nimelaaniwa?

Mpaka siku moja tulikuwa kanisani na mchungaji alihubiri kuhusu baraka, na nikapata kuelewa kitu. Unajua inawezekana kuwa sio kwamba tu tunaamini ni haki yetu kubarikiwa kwa vile sisi ni watakatifu, lakini pia tunaamini baraka zetu ni za ina fulani. Yani tunazo kichwani, mfano : magari, majumba makubwa, pesa nyingi nk.

Wow!

Nahisi kuna matatizo mengi sana na kufikiri huku. Ngoja nielezee ninachofikiria.

1. Nahisi tunaendelea kutokuona Yale mambo Mungu anatenda kwetu kwasababu tu hajatufanikisha kwa namna ile tunayoona mafanikio ndivyo yalivyo. Kwa vile hajatupa pesa nyingi au magari, kitu ambacho sisi ndio tunaona mafanikio, basi kila siku tunaendelea kuona hatujabarikiwa.

2. Tunahisi mabaya yakitupata basi Mungu katuacha au hayuko nasi, kwani kama angekuwa nasi tusingeyapata.

3. Tunahisi tumelaaniwa, tumemkosea Mungu au hatuna imani ya kutosha pale ambapo tunapitia magumu kwenye maisha.

4. Tunaishi maisha yetu kusubiri Mungu atende, au afanye. Na kila siku tunaishi kwa kusubiri hayo ‘mafanikio’ na kumlilia kuhusu hayo tukisahau kuwa uhai wetu pia ni neema, ni zawadi, ni baraka.

Kitu ambacho nimejifunza sasa hivi, na ninaendelea kujifunza ni namna gani mahusiano yangu na Mungu yataendelea kuwa vizuri, yataendelea kuwa imara na bado nitajiona napendwa na Mungu hata nikiwa kwenye shida. Ni jinsi gani naweza kuwa na furaha ya Bwana ambayo ndiyo nguvu zangu nikiwa na shida na nikiwa na raha. Ni jinsi gani niache kujiona kuwa nastahili mema ninayopata na nianze kuyachukulia kama zawadi kutoka kwa Mungu, kwasababu ukweli ni kwamba sistahili chochote, vyote nimepata kwa neema.

Na yote nitakayoyapitia kwenye maisha ni kwa utukufu wake, kwani kuishi ni Kristo, na pia amesema tusiwaze kuhusu kesho, nipo kwenye mikono salama. Maisha yangu ni kwaajili yake.

Yohana 17: 15 – Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu shetani.

Eunice

5 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป